Ankal akiwa na Haji S.Manara
Mkuu wa habari wa Simba leo jijini Dar es salaam
Tarehe 26-9-2015 jana jumamosi kulifanyika mechi ya ligi kuu ya vodacom Tanzania bara baina y a klabu yetu ya Simba na timu ya Yanga. Kwenye mchezo huo timu yetu imepoteza mchezo huo kwa kufungwa goli mbili kwa bila.
Tumeanza kuandika hvyo hapo juu kwa maksudi kuonyesha sisi Simba tumeyakubali matokeo hayo ya dakika tisini za mchezo na tutumie nafasi hii kiungwana kabisa kuwapongeza watani wetu wa jadi kwa ushindi huo walioupata.
Pili tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kumaliza mchezo huo salama. Hapa Mungu ashukuriwe sana pamoja na wapenzi wetu pia. Sababu washabiki wetu wameonyesha utulivu wa kiunamichezo kwa kutokufanya fujo yoyote licha ya mwamuzi wa mchezo huo Israel Nkongo kuharibu mchezo kwa makusudi.

Refa Nkongo kwa dhamira ya kusudi jana aliamua kuwatoa wachezaji wetu mchezoni kwa kuanza kugawa kadi kwa wachezaji wetu pasi na sababu na tena kwa rafu zilezile kuacha wachezaji wa Yanga kucheza bila kuwaonya.
Kilichoshangaza washabiki wote waliokuwa uwanjani na walioangalia kwenye televisheni ni kumuacha mchezaji wa Yanga Donald Ngoma kuendelea na mchezo ilhali alimpiga kichwa cha maksudi mchezaji wetu Hassan kessi!!
Mbali ya vitendo hvyo wachezaji wetu wametulalamikia kutukanwa na mwamuzi wa mchezo huo Nkongo..
Tunaamini Tff watachunguza malalamiko yetu na kuchukua hatua stahiki kwa mwamuzi huyo ambaye kila mtu aliyeuona mchezo huo anakiri kuwa alishindwa kuumudu..
Mwisho na kwa umuhimu wa kipekee klabu ya Simba inaendelea kuwashukuru washabiki kwa utulivu wao licha ya vitendo vya mwamuzi huyo ambavyo vingeweza kabisa kuharibu amani iliyokuwepo uwanjani jana.
Tunawaomba waendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho uongozi wenu umewaandikia TFF na bodi ya ligi ambazo tunaamini zitatenda haki..

Reclaming our glrory
Simba nguvu moja


Imetolewa na Haji S.Manara
Mkuu wa habari wa Simba
Simba sports club
27-9-2015


Nb.mchezo dhidi ya yanga ushapita na sasa tunajipanga kwa game ijayo.
Tunawaomba wapenzi wetu mjitokeze kwa wingi kwenye mechi yetu dhidi ya Stand united jtano ijayo ya tarehe 30-9-2015
👍👌👆☝☝Pamojaaaa. Sanaaa tuu!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ebwana nyie mnafanana hasa hizo pua , ongeeni na madingi wenu inaweza kuwa ni mtu na kaka yake

    ReplyDelete
  2. Acha kulialia wewe......kama kada na chama chao wao kila kitu nongwa ....ukivaaa gwanda tabu, mkikusanyika tabu, ukisema ukae ulinde chako tabu basi wapo wapo tu shiiiiiiiiiiiiiida.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...