Chama Cha Mapinduzi hii leo kimerusha Helikopta yake ya kwanza inayozunguka kwenye kila pembe ya nchi kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu kwenye nafasi zote za Udiwani,Ubunge na Urais. Kazi ya kupasua anga hilo linaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Ushindi Field Marshall  Mwigulu Nchemba ambaye katika Jimbo lake la Iramba kwa asilimia 98 amejihakikishia Ushindi wa kishindo. 
 Makada imara wa CCM  Field Marshall Mwigulu Nchemba na Dkt. Hamis Kigwangalla waki-Magufulika kuonesha sapoti kwa Mgombea wao Dkt. John Pombe Magufuli aliyefanya tukio hilo siku si nyingi kwenye Jukwaa la Kampeni.
Field Marshall Mwigulu Nchemba akilakiwa kwa nderemo mjini Nzega
Dkt Hamisi Kigwangalla akiwasili kwenye Ufunguzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Nzega Mjini.Mjumbe wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi Field Marshall Mwigulu NChemba ambaye  ameanza safari za Anga-kwa-Anga kusaka kura Nchi nzima,Hapa akizungumza na Wananchi wa Nzega namna CCM ilivyosimamisha Mgombea Bora wa Urais ambaye sifa yake kuwa ni KAZI TU na rafiki yake Mkubwa ni TANZANIA. Comrade  Mwigulu amesema, Uchaguzi wa mwaka 2015 ni mwepesi sana kwa CCM  kwa kuwa wagombea wote ni zao la Chama tawala  na wanawajua vizuri. 
 Mbunge Ubunge wa jimbo la Nzega Mjini Ndg. Hussein Bashe akizungumza na Wananchi wake wakati wa Ufunguzi wa kampeni kwa Jimbo la Nzega Mjini. Bashe amewaomba Wana-Nzega kumpatia ridhaa ya kuwa mbunge wa Jimbo hilo ili aweze kusimamia vyema shughuli za Maendeleo kama Uimarishaji wa Huduma za Afya kwa Hospitali ya Nzega, Kusimamia haki za Bodaboda na Mamantilie wa Nzega, shughuli za Halmashauri ya Mji wa Nzega kwa Ufanisi.Pia amesisitiza yeye ni TEAM MAGUFULI na anaamini Maendeleo ya kweli na ya kasi yataletwa na Magufuli kwa awamu hii ya tano ya Uongozi wa Taifa letu.Mbunge Mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi Jimbo jipya la Nzega Vijijini Dkt. Hamis Kigwangala akisalimiana na Wananchi wa Nzega mjini alipokwenda kusapoti Ufunguzi wa kampeni za Mgombea Jirani Ndg.Hussein Bashe. Picha zote na Sanga Festo Jr. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mwegulu Nchemba!

    Nimekuaminia wewe ni AIR MARSHALL. Umeshaongoza mapambano na utuongoze zaidi na zaidi. Hakuna asyekubali. I salute you and behind you weare coming. CCm Oyeeeee!!

    ReplyDelete
  2. Tutumie majina na vyeo vya watu vizuri,...

    Mwandishi sidhani kama unaelewa vema maana ya "Field Marshal"..
    Licha ya kuwa umekosea herufi zake.

    ReplyDelete
  3. Inajionyesha dhahiri kabisa, takriban 99.5% wapo tayari kabisa kwa style ya 'ku-MAGUFULI-ka' kwa nia na moyo mmoja, bila kushawishiwa na mtu yeyote, zaidi ya kuridhishwa, kufurahishwa, kupendezwa na kukubalika kwa sera za wazi kabisa zinazoendelea kunadiwa katika kampeni mbali mbali kuelekea uchaguzi mkuu siku chache zijazo. Mola tujaaliye uchaguzi wa salama na amani In Sha Allah. Ameen.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...