SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), imezindua rasmi mfuko wa akiba na mikopo (Saccos) kwaajili ya wafanyakazi wa shirika hilo katika harakati za kujikomboa kiuchumi na kuimarisha umoja miongoni mwao.

Akiongea na wafanyakazi katika uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja amewahimiza wafanyakazi kuitumia Saccos hiyo kujikomboa kiuchumi na kuondokana na utozwaji mkubwa wa riba kutoka kwa baadhi ya taasisi za fedha, hali inayowaumiza watumishi wengi nchini.

Uanzishwaji wa mfuko huo umelenga kuwasaidia wafanyakazi kutatua matatizo ya haraka yanayojitokeza ndani na nje ya maisha ya kazi na kuiweka Saccos hiyo kama sehemu ya Dawasco kujipanua zaidi katika kujali maslai ya wafanyakazi wake.

Saccos ya Dawasco imezinduliwa ikiwa na mtaji wa kuanzia wa Tsh Milioni 95 na jumla ya wanachama736 huku Ndugu Ramadhani Mtindasi akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Saccos hiyo na nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikienda kwa Erasto Emmanuel.

Mara baada ya uchaguzi huo, viongozi hao wamehaidi kuleta mapinduzi na mabadiliko ya uendeshaji wa mfuko huo kwa kuhakikisha unatoa unafuu kwa kila mwanachama na kuweka masharti rafiki ili kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...