Mkurugenzi
wa Elimu ya juu kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi,
Prof. Sylivia Temu akizungumza wakati wa uzinduzi mradi wa ujenzi wa
kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya moyo hapa nchini
uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kituo hicho kitakachokuwa na
uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa
nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kitakuwa chini ya usimamizi
wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS).
Mkurugenzi
wa Elimu ya juu kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi,
Prof. Sylivia Temu (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na
uongozi wa chuoChuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha
Muhimbili (MUHAS), wawakilishi kutokakutoka Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya afya baada
yauzinduzi
mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya
moyo hapa nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kituo hicho
kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye
magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kitakuwa
chini ya usimamizi wa (MUHAS).
Na Mwandishi wetu,
SERIKALI
imezindua mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na
mishipa ya moyo hapa nchini kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za
kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa
Afrika mashariki.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana
kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Bw. Shukuru
Kawambwa, Mkurugenzi wa Elimu ya juu nchini, Prof. Sylivia Temu alisema
mradi huo unaotekelezwa na serikali kwa ushirikiano na benki ya
maendeleo ya Afrika ni
mojawapo ya miradi minne ya afya inayotekelezwa kwenye ukanda wa afrika
mashariki ikilenga kutatua changamoto mbalimbali za kiafya.
“Kila
nchi ya Afrika Mashariki ina mradi wa aina yake kwenye sekta hii muhimu
na kwa upande wetu sisi umejikita katika kukabiliana na magonjwa ya
moyo na utakuwa chini ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) na
utakwenda sambamba na ujenzi wa kampasi mpya ya chuo hicho unaondelea
huko eneo la Mloganzila hapa jijini Dar es Salaam,’’ alibainisha.
Akizungumzia
faida za mradi huo Prof Temu alisema utasaidia kupunguza vifo
vitokanavyo na magonjwa ya moyo hapa nchini sambamba na kupunguza
gharama zinazolikabili taifa kwa sasa kutokana na kusafirisha idadi
kubwa ya wagonjwa wa moyo kwa ajili ya kutafutaa matibabu nje ya nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...