Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo, baada ya kukaa kimya kingi sana tangu mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia  Chama cha Demokrasia na Maendeleo  chini ya mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kuhamia chama hicho. Leo ameibuka na kusema  ya moyoni kuwa amejivua uanachama  rasmi wa chama cha Chadema pamoja na Ukatibu Mkuuu wa Chama hicho na kuachana  kabisa na siasa  kutokana na mambo yaliyokuwa yakifanyika ndani ya chama chake hayakumridhisha na hakukubaliana nayo.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa pia amesema kuwa mambo yaliyotokea katika chama chake ndio maana ameamua kuachana na siasa  rasmi hii leo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kupata taswira nzuri za aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.





Baadhi ya wananchi pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dk.  Wilbroard Slaa leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Siasa kama hizi ni mbaya sana angekuwa na hekima kidogo angenyamaza mpaka uchaguzi upite ndiyo aongee huu upuuzi. Hata sasa hakuna anayemkumbuka Kabisa, kitendo hiki kinadhihirisha yeye ndiyo aliyeutaka urais kuliko hata ENL.

    ReplyDelete
  2. Amesema ukweli kabisa. Alishamponda wakati Lowasa yupo CCM na si yy pekee yake viongozi karibu wote ndani ya chama cha chadema nccr cuf kwa kumwita fisadi namba moja. Sasa leo I weje ale matapishi yake. Na ingekuwa Lowasa au Sumaye mmoja wao angechaguliwa kuwa mgombea Urais kupitia CCM wangekuja Chadema? Na kama kweli CCM mbaya kwao kwa nini miaka yote hawakujiengua? CC wananchi tutumie akili na Fikra zetu kujua nani anafaa au nani hafai. Sijasema kama CCM Ni nzuri au mbaya Ila viongozi kama Lowasa na Sumaye kwangu naona Ni wanafik.

    ReplyDelete
  3. Ni vizuri kusema ukweli kuliko kunyamazia mambo yanayoweza kukuumbua baadaye. Usiwe na jazba mdau wa kwanza acha propaganda ungekuwa wewe Dr Slaa ungengoja?

    ReplyDelete
  4. Nilikuwa namchukia slaa kumbe nilikuwa nakosea, Mungu amjaalie hekima na busara zaidi

    ReplyDelete
  5. ni kweli kabisa, yote hayo ni uchu wa madaraka tu anayo na uongozi wenyewe ungekuwa shida, kama dili ilimshinda, ndoa ikamshinda, ccm ikamshinda, chadema ikamshinda, KUONGOZA TAIFA NDO ANGELIWEZA KWELI JAMANI? hainiingii akili, sasa ni ccm B.
    hata lolote, MH. RAIS LOWASA MBELE KWA MBELE, kurudi nyuma haturudi, kusikia la yeyote yule hatusikii, yaani sisi ni atuambilikiii, UKAWA mbele kwa mbele, penda usipende Lowasa ni rais awamu ya tano.
    hakuna jipya kila agenda mnayozungumzia ni RICHMOND tu, je hizo zingine kibao mbona hamzisemi km EPA, KAGODA,DEEP GREEN, MEREMETA, RADA, NBC, SUKARI, MABEHEWA FEKI, ESCROW, NYUMBA ZA SERIKALI NAKADHALIKA, kwamba hamzioni, hamzijui au ni kukosa sera za kuwapa wananchi. Toeni sera acheni zenu hizo za chuki binafsi, mnakubali ccm kushindwa hata kabla ya uchaguzi. kaaz kweli kweli.
    Peoplezzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz

    ReplyDelete
  6. Sina chama cha siasa, lakini wakati wa kuanza kampeini za Uchaguzi Mkuu - kwa Katibu Mkuu wa chama kikubwa cha upinzani(Chadema)anapotofautiana na mediocre Mwenyekiti wake (ambaye hana sifa za kuweza kudiriki kuwa mtangazania wa kuwania cheo cha urais nchini; kwa Mwenyekiti wa Chama kingine cha upinzani (Lipumba wa CUF) kujiuzulu na huku wote ndio walikuwa mbele katika Ukawa; na Ukawa kupata candidate kutoka chama tawala ambacho walisema kuwa ni kabila la kuzalisha masisadi (Tundu Lissu) na kwamba ni mashetani (Freeman Mbowe) ni vioja vya ajabu sana katika siasa za Tanzania. Sijui wanatupelea wapi na huyu Lowassa ambaye sasa wanarudi kula matapishi yao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...