
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe
Magufuli akitoa mpya jukwaani jana kwa kupiga Push Up kama kumi hivi ili
kuwadhihirishia wananchi wa Mjini Karagwe mkoani Kagera kuwa yuko fiti
kiafya ili kuwatumikia watanzania mara watakapompa ridhaa ya kuwaongoza Watanzania ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika
uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani .
Huku umati wa Wakazi wa Karagwe ukishangilia kwa mayowe,Dkt Magufulia alieleza kuwa kazi ya
kuwatumikia Watanzania siyo rahisi ni muhimu kuwa na afya njema ili
kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na yuko tayari kuwatumikia Watanzania kwa kufanya kazi usiku na
mchana.
Wananchi wa mji wa Ngara na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya posta mjini humo,huku wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais na kuiongoza nchi Tanzania katika awamu ya tano.Dkt Magufuli amekamilisha mikutano yake ya kampeni zake katika mkoa wa Kagera wenye jumla ya majimbo 9 ya Uchaguzi.
PICHA NA MICHUZI JR-KAGERA
PICHA NA MICHUZI JR-KAGERA
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Posta,wilayani Ngara jioni ya jana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.Dkt Maguful kwa siku mbili mfululizo ameweza kukamilisha mikutano yake kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Kagera,ambapo kesho anaelekea mkoani Geita kwa ajili ya kujinadi kwa wananchi wa mkoa huo ili waweze kumpigia ya kuwa Rais wa awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwafafanulia kwa umakini mkubwa alipokuwa akiwahutubia wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyerwa mapema jana mchana mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Sehemu ya umati wa watu ulikuwa umefika kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli uliofanyika mapema jana mchana kwenye uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyera mkoani Kagera.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyerwa mapema jana mchana mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Hahaha!!! this is really funny. Sijawahi kuona mgombea urahisi akizichapa push-up tena za ngumi ili kuonesha fitness level yake. This is really great. Sasa tunaomba tuone na kumi za Mr. Lowasa pia. Halafu Mr. Museveni next year (2016) na Kagame the following year (2017). Mambo matamu haya in East Africa.
ReplyDeleteNaye Tyson! Tunataka Kiongozi atakae weza kufumua uozo ulioko Tanzania
ReplyDeleteLowasa akizipiga push up kumi ataenda ICU Muhimbili na uchaguz unaahirishwa!! Hahahahah!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteMy President magufuli
ReplyDelete