1
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mpya jukwaani jana kwa kupiga Push Up kama kumi hivi ili kuwadhihirishia wananchi wa Mjini Karagwe mkoani Kagera  kuwa yuko fiti kiafya ili kuwatumikia watanzania mara watakapompa ridhaa ya kuwaongoza Watanzania ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani .

Huku umati wa Wakazi wa Karagwe ukishangilia kwa mayowe,Dkt Magufulia alieleza kuwa  kazi ya kuwatumikia Watanzania siyo rahisi ni muhimu kuwa na afya njema ili kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na yuko tayari kuwatumikia Watanzania kwa kufanya kazi usiku na mchana.
2
 Wananchi wa mji wa Ngara na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya posta mjini humo,huku wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais na kuiongoza nchi Tanzania katika awamu ya tano.Dkt Magufuli amekamilisha mikutano yake ya kampeni zake katika mkoa wa Kagera wenye jumla ya majimbo 9 ya Uchaguzi. 
PICHA NA MICHUZI JR-KAGERA
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Posta,wilayani Ngara jioni ya jana  kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.Dkt Maguful kwa siku mbili mfululizo ameweza kukamilisha mikutano yake kwenye Wilaya  zote za Mkoa wa Kagera,ambapo kesho anaelekea mkoani Geita kwa ajili ya kujinadi kwa wananchi wa mkoa huo ili waweze kumpigia ya kuwa Rais wa awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwafafanulia kwa umakini mkubwa alipokuwa akiwahutubia wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyerwa mapema jana mchana mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Sehemu ya umati wa watu ulikuwa umefika kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli uliofanyika mapema jana  mchana kwenye uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyera mkoani Kagera.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyerwa mapema jana  mchana mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hahaha!!! this is really funny. Sijawahi kuona mgombea urahisi akizichapa push-up tena za ngumi ili kuonesha fitness level yake. This is really great. Sasa tunaomba tuone na kumi za Mr. Lowasa pia. Halafu Mr. Museveni next year (2016) na Kagame the following year (2017). Mambo matamu haya in East Africa.

    ReplyDelete
  2. Naye Tyson! Tunataka Kiongozi atakae weza kufumua uozo ulioko Tanzania

    ReplyDelete
  3. Lowasa akizipiga push up kumi ataenda ICU Muhimbili na uchaguz unaahirishwa!! Hahahahah!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...