SERIKALI imetwaa jumla ya Ekari 7000 baada ya ubatilishwaji wa Mashamba ya Tanzania plantatition limited yaliyokua yakimilikiwa na mwekezaji  kutoka nje ,mashamba hayo yanatajiwa kugawanywa kwa wananchi 2000 wenye uhitaji wa ardhi ya makazi na mashamba .

Aidha baada ya ubatilishwaji wa mashamba hayo Arusha imepata ekari 6176.5 na Halmashauri ya Meru ekari 925  hivyo kufikia ekari 7101 ambazo zitagawanywa kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi,Wiliam Lukuvi wakati akitoa taarifa ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi  katika mikoa ya Arusha na Manyara katika mkutano wake na Waandishi wa Habari,Lukuvi amesema kuwa mashamba hayo yalikua na migogoro kwa kipindi kirefu kati ya mwekezaji na Wananchi hivyo kutokana na uhitaji mkubwa wa ardhi serikali imeamua kubatilisha mashamba hayo.

“Nimekuja Arusha na timu yangu ambayo itafanya uhakikiki wa watu 2000 wenye uhitaji na baada ya kujiridhisha watafanya zoezi la ugawaji na pia wananchi watapatiwa hati ya kumiliki ardhi zao safari hii hatutagawa ardhi kienyegi” Alisema Lukuvi

Lukuvi amesema kuwa mbali na shamba hilo pia wamepata ekari 100 katika shamba la Imani Estate na pia Shamba la Noors  lenye Ekari 2296  lililokua na mgogoro kati ya Mwekezaji na wananchi wa Kijiji cha Laroi na Kisima cha Mungu litagaiwa kwa wananchi baada ya mazungumzo kati ya Mwekezaji kukubali kuachia shamba hilo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC ,Fidelis Lumato amesema kuwa ugawanywaji wa mashamba hayo utasaidia kupunguza migogoro mikubwa ya ardhi iliyokua inakabili wilaya hiyo kutokana na uhaba mkubwa wa ardhi.

Jumla ya migogoro 80 iliyowasilishwa kwa Waziri Lukuvi kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Arusha ,Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na Halmashauri ya Meru imepatiwa ufumbuzi hivyo kupunguza migogoro ya ardhi ilikua ikilisakama jiji la Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Safi mzee lukuvi na timu yako. Muzunguke nchi nzima mufanye hivyo

    ReplyDelete
  2. Mashamba kuwa makazi!, naona sera ingekuwa wananchi wangepewa ardhi hiyo kwa masharti ya kuwa wafanye ardhi hiyo iwe ya kilimo bora ili kulinda ardhi zinazofaa kwa kilimo kitacho zalisha mazao ya chakula kwa wingi na ziada kuuza kujiingizia kipato na siyo kugeuza ardhi kuwa makazi.

    Mdau
    Christos Papachristou
    Diaspora.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...