KWA WASUKUMA WOTE DUNIANI
Kijana FRANK MASANJA (akiwa na mama yake pichani) anamtafuta baba yake mzazi aitwae MASANJA BASU.  Masanja alikuwa anaishi kwa kaka yake aitwae SHINGERA BASU sehemu iitwayo NYAKATO SOKONI mkoani MWANZA, Kabila la Masanja ni msukuma wa mkoani Shinyanga wilaya ya Bariadi katika kijiji kiitwacho BUDARABUJIGA na jina la ukoo wao ni BASU. 

Sasa hivi wilaya ya Bariadi ipo ndani ya mkoa mpya wa Simiyu na si Shinyanga tena.

 Mke wa kaka yake alikuwa mwalimu wa shule ya msingi. Baadhi ya watoto wa kaka yake ni BUSARU na MAEGA.

Masanja na kaka yake awali walikuwa wakiishi Shinyanga na kuamia Mwanza na kuwa wanafanya biashara ya madini wakiyafuata Nyarugusu, Singida Manyoni, Geita na sehemu zingine nyingi. 

Masanja alikutana na mama wa mtoto huyo aitwae SIWEMA ZABRON aliyekuwa akiishi kwa shangazi yake aitwae mama Jumanne sehemu iitwayo MEKO hapohapo mkoani Mwanza na mwaka 1995 Frank akazaliwa.

Frank alikwenda kumtafuta baba yake mwaka jana (2014) huko nyakato sokoni na kukuta nyumba waliokuwa wakiishi baba yake imeuzwa na kuambiwa kuwa wameamia Dodoma. Frank kwa sasa anaishi jijini Dar es salaam na mama yake.

Kwa yoyote anayemfahamu au kumfahamu mtu yeyote aliyetajwa hapo juu au kumjua mtu aliyekaribu na ukoo huo anaombwa kumsaidia kijana huyo aweze kumpata baba yake.
Asanteni na Mungu awabariki.
Mawasiliano
Namba za simu za mama Frank
+255 654 092813 au +255 755 451213
Namba za whatsapp za Frank +255 716627814

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Pole kijana,kila la kheri ummpate baba yako naye pia awe na hamu ya kukuona. Hii inachangiwa sana na sharia za bongo land, ati motto akizaliwa nje ya ndoa basi baba halazimiswhi kutoa matunza. Midume inazalisha halafu ina toka "benzi". Badilisha sharia hii na wababa walipe matunzo ya watoto wao, siyo kufaidi "uroda" tu halafu wanatoka baruti kutunza matokeo ya "uroda" waliokula kwa ridhaa yao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...