Klabu ya soka ya Simba kwa kushirikiana na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo zimezindua huduma mpya inayojulikana kama ‘Pata habari za klabu ya Simba’ ambayo itawawezesha wateja wanaotumia mtandao wa Vodacom kupata habari zinazohusiana na klabu ya Simba popote watakapokuwa hapa nchini.
Kampuni nyingine shirika katika kufanikisha huduma hii ni Premier mobile solution na EAG Group.
Kampuni nyingine shirika katika kufanikisha huduma hii ni Premier mobile solution na EAG Group.
Huduma hii mpya ya ‘Pata habari za klabu ya Simba’ni rahisi na ya ufanisi mkubwa kuwawezesha wateja kupata habari kwa haraka “Kutokana na kukua kwa sekta ya TEKNOHAMA Vodacom inaelewa umuhimu wa kuwapatia wateja wake taarifa wanazohitaji kuzipata kwa haraka na ndio maana leo imeshirikiana na klabu ya Simba na kampuni ya PMS kuanzisha huduma hii inayowawezesha wateja wetu kupata habari za papo kwa papo na zenye uhakika wakati wowote kupitia simu zao za mkononi”.Amesema Kelvin Twissa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania.
mtandao wa Vodacom kupata habari motomoto na za papo kwa hapo kupitia simu Kwa upande wake msemaji wa Klabu ya Simba na Rais wa klabu hiyo Evans Avena amesema
“Tuna imani huduma hii ni ubunifu wa aina yake ambao utakaowawezesha wapenzi wa klabu ya Simba na wapenzi wote wa mchezo wa soka ambao wanatumia zao za mkononi”.
“Tuna imani huduma hii ni ubunifu wa aina yake ambao utakaowawezesha wapenzi wa klabu ya Simba na wapenzi wote wa mchezo wa soka ambao wanatumia zao za mkononi”.
“Tunatoa wito kwa washabiki wetu na wapenda soka kujiunga na huduma hii ambapo watakuwa wanapata habari za papo kwa papo kuhusiana na Simba kutoka vyanzo vya habari vya kuaminika”.Alisema Aveva.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group ambayo pia ina mbia katika huduma hii Imani kajula,alisema kuwa huduma za namna hii zinawarahishia maisha kwa kupata habari motomoto wateja wanaotumia mitandao ya simu kama ambavyo Vodacom itatumia mtandao wake kuwafikishia habari motomoto za klabu wa Simba kwa wateja wake.
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Premier Mobile Solution Lulu Ramole alissema huduma hii ya aina yake itarahisisha wapenzi wa habari za michezo kupata habari za motomoto kupitia mtandao wa Vodacom kwa gharama nafuu ambapo mteja atatozwa shilingi 150 kupata huduma hii kwa siku na fedha hizo zitakatwa kwenye salio lake la muda wa maongezi.
Kupata huduma hii mteja anatakiwa kutuma neno SIMBA kwenda namba 15460 na baada ya kutuma ujumbe atapokea ujumbe wa kumfahamisha kuwa amejiunga na atakatwa na kuendelea kupokea habari na kupitia huduma hii mteja anaweza kupata habari za klabu ya Simba kuanzia tatu na kuendelea kwa siku.Iwapo mteja atataka kujiondoa kuitumia huduma atatakiwa kuandika neno ONDOA SIMBA kwenda namba 15460.
Kwa taarifa zaidi wanaweza kupata kwenye websiteya Simba www.simbasports.co.tz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...