Msajili Msaidizi
wa ofisi ya msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akizungumza na
waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kuufahamisha umma kuwa chama cha siasa Tanzania Peoples Party (TPP)
kilifutwa kwenye orodha ya vyama vya siasa hapa nchini na chama hicho hakipo kwenye orodha ya vyama vya siasa vilivyopo hapa nchini amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo, kushoto ni Mkurugenzi Utawala na Rasilimali watu Emmanule Kayuni,.
Wanahabari wakimsikilza kwa makini Msajili Msaidizi wa ofisi ya msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza leo Jiji Dar es
Salaam.
(Picha na Emmanue Massaka).
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa
imesema kuwa Chama cha Tanzania People’s Party (TPP) kilifutwa, hivyo hakuna mtu
mwenye mamlaka ya kutumia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Akizungumza na waandishi habari leo
jijini Dar es Salaam, Msajili Msaidizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa, Sisty Nyahoza amesema kuwa hivi karibuni kuna watu wameonekana katika
chombo cha habari kimoja sio Michuzi, wakiwajinasibu katika chama cha TPP wakati chama hicho
kilishafutwa toka 2001.
Nyahoza amesema kuwa watu wanaotumia
chama hicho sheria itashika mkondo wake kwa kuwachukulia hatua watu kutumia
chama ambacho kilishafutiwa usajili wa kudumu kwa msajili wa vyama vya siasa.
Aidha amesema kuwa vyama vilivyo
katika usajili wa kudumu na vimeshiriki uchaguzi mkuu ni vyama 22 hivyo watu
watambue chama cha TPP kilishafutwa kutokana na kukiuka kwa taratibu za ofisi
ya msajili wa vyama vya siasa.
Nyahoza amesema kuwa watu
wote wanaotumia vyama ambavyo usajili wake ulishafutwa kwa mamlaka ya ofisi ya msajili wa vyama vya
siasa watatachukuliwa hatua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...