SHIRIKA la Majisafi
na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limewatahadharisha wananchi kuepuka taarifa
za uzushi zilizoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari juu ya usambazaji maji
machafu kwenye line za mabomba ya wateja wa Dawasco.
Akizungumza na gazeti
hili, Kaimu Meneja Uhusiano wa Dawasco , Bi Everlasting Lyaro alisema taarifa
hizo za uzushi zimesambazwa na watu wachache ili kuchafua taswira ya shirika
hilo na pia kuihusisha Dawasco moja kwa
moja na mlipuko wa kipindupindu ulioingia jijini.
“Tunawatahadharisha
wateja wetu kuwa ubora wa maji unaozalisha na Dawasco unakidhi vigezo vyote kwa
matumizi ya binadamu na viumbe hai, hatuwezi kuzalisha maji yenye kuleta
madhala kwa wananchi kwani hata haki za binadamu haziruhusu kufanya hivyo ”
alisema Lyaro.
‘Ukweli wa maeneo
yanayolalamikiwa kama vile Ilala mitaa ya Sharif shamba na Buguruni ni kuwa
kuna kampuni za uchimbaji mifereji bado hatujabaini kama ni ya watu binafsi au
za manispaa.
Wao walichimba mifereji ya majitaka karibia na mabomba ya wateja
walio na line za Dawasco za majisafi hivyo kutiririsha majitaka kwenye mfumo wa
majisafi. Ikapelekea maji machafu kuingia kwenye line zao na kupelekea mabomba
ya maji yanapofunguliwa zinakutana na yale maji machafu yaliyokatwa kutoka
kwenye mifereji” aliongezea lyaro.
Alisema kuwa Baada ya
kupokea malalamiko hayo tulichukua hatua kadhaa moja ni kuchukua sampuli za Maji
hayo na kwenda kuyapima na kurudi kufunga maji hayo yasiendelee kutoka. Na baada ya upimaji sampuli ile na kukuta sio
salama tulitenga line(isolate) ya majisafi ya sharif shamba hadi hapo tatizo
litakapotatuliwa na mamlaka husika.
Tuhuma za Dawasco
kusambaza Maji machafu ziliripotiwa mapema wiki hii huku zikihusishwa zaidi na
athari za ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea kushika kasi jijini dar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...