Good people,
I understand that some of you will have seen or heard about a disturbing message on WhatsApp about all data communications being closed during the election period.

Please rest assured that the message is a hoax.

On JamiiForums, someone has offered an excellent analysis as per hereunder.  You are welcome to copy and paste it that text as a response to anyone who propagates the hoax.  

The original message can be found at
 the link, where the hoax alert is also quoted.

Cheers,
DS.

=============================

KUHUSU: Taarifa inayosadikiwa kutoka kwa "Rene Meeza, Mwenyekiti wa umoja wa makampuni ya mawasiliano Tanzania".

Kwenye JamiiForums, kuna mtu aliyejisajili ya jina la "Mdanganywa", ambaye amejibu vizuri ifuatavyo:
-------
http://www.jamiiforums.com/showpost.php?p=14037211
Mtoa maelezo,

1: Kwanza jina la huyo jamaa anaitwa Rene Meza na siyo Rene Meeza

2: Nijuavyo mimi Rene Meza hajui kiswahili ni mtu wa nchi moja huko South America, sijui ni Colombia au Venezuala.

3: Rene Meza alitangazwa kwamba ameshaacha kazi hapa nchini na nafasi yake imechukuliwa na jamaa anaitwa Ian Ferrao.

4. Taarifa yako imeandikwa tarehe 19.09.2015 wakati leo ni 18.09.2015.

5. Umoja wa Makampuni ya simu hata hukutaja unaitwaje walau kwa kifupi

6. TCRA au taasisi ya serikali, haitumi taarifa kwenye Umoja. Umoja ni kitu ambacho hakiko registered. Ni kama ambavyo NEC haiwezi kutuma taarifa kwenye UKAWA maana UKAWA haijasajiliwa. Hivyo, taarifa zote hutumwa kwenye kampuni zote hata kama itakuwa ni barua moja itachapwa ileile na wanabadilisha addressee. hata kama makampuni yako 1,000 kila kampuni itapata barua yake binafsi

7. Kama ni taarifa ingetoka moja kwa moja TCRA au NEC kwenda kwenye vyombo vya habari na si kwingineko

8. Agizo lolote la kisheria hutamka kifungu cha sheria kinachotumika kuweka katazo hilo, barua yako haina kifungu chochote.

9. TCRA ni chombo huru kama ilivyo NEC haipati maelekezo toka NEC. TCRA wanafanya kazi kwa mujibu wa Sheria ya TCRA na zingine kama Electronics, na si vinginevyo.

10. Leseni za makampuni hazina kifungu kinachokataza kufanya biashara kwa sababu ya uchaguzi, unataka kusababisha wapelekwe ICC.

Kajipange upya kutuelezea
--------

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...