Na Bashir
Yakub
Kama ilivyo makubaliano
katika shughuli nyingine
za kijamii ajira
nayo huwa na makubaliano maalum
wakati inapoingiwa.
Makubaliano haya ndiyo
huitwa mkataba na yumkini
huingiwa kati ya
wahusika wawili yaani
muajiriwa na muajiri.
Aina
ya mahusiano wanayoingia
wahusika ndiyo huibua
aina za haki na wajibu
kwa pande zote
mbili. Mwenye haki hutakiwa
kutoa haki hiyo
kwa mwenzake naye
mwenye wajibu huwa
hana hiari isipokuwa kutekeleza
wajibu huo kwa
mujibu wa makubaliano.
Hapa
Tanzania taratibu za
ajira na mahusiano
kazini huongozwa na
Sheria namba 6 ya
ajira na mahusiano
kazini 2004. Sheria hii
hueleza wajibu, haki,
stahili, kuacha na
kuachishwa kazi na
kila kitu kinachohusu
ajira na kazi
kwa ujumla wake. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...