FieldMashall Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Sikonge hii leo Mkoani Tabora wakati wa Mkutano wa Kampeni wa Chama Cha Mapinduzi,Mwigulu Nchemba amewasisitiza Wananchi wa Sikonge Kuachana na siasa za Makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi,"Wananchi wote,WanaCCM wote tuunganishe nguvu zetu kukipa Ushindi chama cha Mapinduzi,Tuunganishe nguvu kuhakikisha tunapata Mbunge wa CCM atakayeweza kutatua Matatizo ya Tumbaku hapa Sikonge"
Mbali na hilo ,Mwigulu Nchemba ameendelea kusisitiza Uchaguzi wa Amani na Upendo kwa vyama vyote,Amewasihi Wananchi wajitokeze kupiga Kura ilikuwachagua Madiwani,Mbunge na Rais wa Chama cha Mapinduzi wenye Ilani inayotekelezeka.
Mjumbe wa timu ya Ushindi ya CCM Taifa Comrade Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Jimbo la Igagula Ndg.Ntimizi hii leo alipofika kwaajili ya kuinadi Ilani ya CCM na kuwasihi Watanzania walipojo Tabora kuichagua CCM kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwishoni mwa October 2015.
Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sikonge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.Said Nkumba aliyekuwa Mbunge wa sikonge akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la sikonge kuuonesha wazi Umma kuwa CCM kwa Sikonge ni Moja.Vijana wa kazi wa Chama Chama Mapinduzi Ndg.Mwigulu Nchemba na Hamis Kigwangalla wakionesha Umahili wao wa kupiga Push-Up kabla ya Kuanza kwa Mkutano wa hadhara Jimbo la Sikonge hii leo Mkoani Tabora.Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Jimbo la Sikonge waliofurika kusikiliza sera za Chama cha Mapinduzi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.
Picha na Sanga Festo Jr. Picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Air MarshallMwegulu na wengine kwenye kamati yetuya ushindi. Tuko pamoja nanyi. Nyinyi mnatuongoza sisi tunamalizia na kufagilia njia!! Waonesheni umahiri wetu physically na pia kisera. Nawahakikishieni hamko wapweke, tupo mahiri nyuma yenu!! Field Marshall Nchemba kazi tumeianza, tuimalizie vizuri kaka. Hebu tuonesheni na umahiri wa kina dada wetu pia!! Kigamboni Mbagala,Kakonko na Ushirombo tupo. Masasi na Msangamkuu pia Rombo na Himo tumejumuika. Monduli na Hai pia Korogwe tunawakilisha. Rungwe na Karagwe pia Uyui tumetulia. Mikindani na Kiwangwa pia Kyerwa tunajali. Magufuli Rais wetu tumeshajipanga kwa maapisho hapo Magogoni. Mwegulu paaa juu,tusomee ramani sisi ardhini tunamalizia. Ha ha haaaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...