TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu
Casmir Kyuki kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria.
Kabla ya
uteuzi huu, ndugu Kyuki alikuwa Mwandishi Kufuatia uteuzi huu, Rais amemteua
Bibi Sarah Barahomoka kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria, kujaza nafasi iliyoachwa
wazi na ndugu Kyuki.
Kabla ya uteuzi huu, Bibi Barahomoka alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya
uandishi wa Sheria. Uteuzi
huu unaanza mara moja.
Wateule
hawa wataapishwa Tarehe 16 Septemba, 2015, Ikulu Dar-es-Salaam leo saa 3 asubuhi.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari, Msaidizi,
Ikulu-DSM
15 Septemba,
2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...