TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu
wawili wapya wa mikoa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wakuu wa Mikoa ambao wanawania
ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa
iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK),
Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa katika uteuzi wake, Rais Kikwete amemteua Ndugu
Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Ndugu Jordan Rugimbana kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Lindi.
Aidha,
Rais Kikwete amewahamisha wakuu wawili wa mikoa – Ndugu Mwantumu Bakari Mahiza aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Ndugu Saidi Magalula
ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitokea Mkoa wa Tanga.
Ndugu
Magalula anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Stella Manyanya anayewania ubunge
mkoani Ruvuma pia.
Ndugu
Makalla ambaye alipata kuwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Morogoro na Naibu Waziri
wa Maji anachuku anafasi iliyoachwa wazi na ndugu Leonidas Gama ambaye anawania
ubunge mkoani Ruvuma.
Ndugu
Rugimbana ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi
kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Mahiza.
Uteuzi
na uhamisho huo ulianza Jumamosi, Septemba 12, mwaka huu, 2015 na wakuu wapya wa
mikoa wataapishwa kesho kutwa Jumatano, Septemba 16, 2015, Ikulu, Dar es
Salaam.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Profesa Muhammed Bakari Kambi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Profesa Muhammed Bakari Kambi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Taarifa
iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK),
Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza tokea Jumatano, Septemba 9,
2015.
Kabla
ya uteuzi wake, Profesa Muhammed Bakari Kambi alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu
cha Tiba na Afya Shirikishi cha Muhimbili, Dar es Salaam.
Vile vile, Rais Kikwete amemteua
Ndugu Mlingi Elisha Mkucha kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa
(NDC). Uteuzi huo ulianza Jumatano, Septemba 9, mwaka huu, 2015.
Taarifa
iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 12, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK)
Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa Ndugu Mlingi Elisha Mkucha ni mwanasheria kwa
taaluma na mwajiriwa wa NDC kwa miaka 14 iliyopita ambako ametumikia katika
nafasi mbali mbali mpaka akawa Kaimu Mtendaji Mkuu.
Ndugu
Mkucha anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Gideon Nassari aliyestaafu kwa
mujibu wa sheria.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua
Dkt. Tulia Ackson kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia Jumatano,
Septemba 9, mwaka huu, 2015.
Kabla
ya uteuzi wake, Dkt. Tulia Ackson ni Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
14 Septemba, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...