Wimbo maalum wa kuhimiza amani kabla na baada ya uchaguzi
mkuu, utawekwa rasmi hadharani mbele ya waandishi wa habari Jumanne hii.
Wimbo huo uliopewa jina la “Amani Kwanza” utapigwa ‘live’
kwa mara ya kwanza mbele ya wana habari ndani ya ukumbi wa nyuma wa Mango
Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam kuanzia saa 6 mchana.
“Amani Kwanza” ni ngoma iliyopigwa katika miondoko ya rhumba
ikiwa imeshirikisha nyota wengi wa muziki wa dansi chini ya umoja wa muda wa wanamuziki wa dansi na taarab.
Mgeni rasmi katika tukio hilo anatarijiwa kuwa mkuu wa
wilaya ya Kinondoni bwana Paul Makonda.
Mratibu wa ‘project’ hiyo Juma Mbizo alisema umoja huo
haufungamani na dini, kabila wala chama chochote na kwamba lengo la ni moja tu
– kusumbaza ‘mahubiri’ ya amani, umoja na mshikamano kabla na baada ya Uchaguzi
Mkuu.
Mbizo amefafanua kuwa wimbo huo umerekodiwa katika studio za
Sound Crafters chini ya producer Enrico huku video ikiwa imefanywa na King
Dodoo.
Wanamuziki waliotengeneza wimbo huo wako chini ya kamati inayoongozwa
na Kanku Kelly ambaye ni mwenyekiti, katibu Omar Teggo, wajumbe ni Mafumu Bilal,
King Dodoo na King Kiki huku Juma Mbizo akiwa mjumbe na mratibu.
Mbizo amesema baada ya utambulisho huo, kila mwanahabari
atapatiwa CD na DVD moja ya wimbo huo.
“Lengo letu ni kutaka wanahabari wawatambue wasanii wote
walioshiriki kutengeneza wimbo huo ikiwa ni pamoja na kuusikiliza ‘live’ hivyo
naomba waandishi wa habari na wadau wa muziki waje kwa vingi Mango Garden Jumanne
mchana,” alisema Juma Mbizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...