Rais Kikwete akifunua pazia kuzindua rasmi majengo majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015
 Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi majengo pacha ya PSPF TOWERS.


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mfano wa kadi yake baada ya kujiunga mfuko wa pensheni wa PSPF kwenye sherehe hizo. Kulia ni Naibu waziri wa Fedha Mhe. Adam Kighoma Malima. Kulia kwa Rais ni Mwenyekiti wa Bodi ya PSPF Mhe. George Yambesi na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF Bw. Adam Mayingu 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka alama ya dole kwenye fomu yake ya uanmachama baada ya kujiunga mfuko wa pensheni wa PSPF kwenye sherehe hizo. Kulia ni Naibu waziri wa Fedha Mhe. Adam Kighoma Malima. Kulia kwa Rais ni Mwenyekiti wa Bodi ya PSPF Mhe. George Yambesi na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF Bw. Adam Mayingu 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na  na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dr. Ramadhani Dau  na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio kwenye sherehe zsa  kuzindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015.


Jengo refu zaidi lililokamilika Afrika 
Mashariki na Kati lazinduliwa nchini Tanzania.


PSPF Towers ni moja ya majengo machache marefu barani Afrika na ndiyo jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa mita 147.
Majengo mengine marefu Afrika ni Carlton Centre (mita 223) lililopo Afrika Kusini, Hassan II Mosque (mita 210) lililopo Moroko, Ponte City (mita 173) lililopo Afrika Kusini, Necon House (Mita 160) lililopo Nigeria, Marble Tower (mita 152), Pear dawn (mita 152), Pear dawn (mita 152), Met Life Centre (mita 150) na 88 on field (mita 147) yote ya Afrika ya kusini.

Jengo hilo lililozinduliwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ujenzi wake uliofanywa na makandarasi wazalendo ulitumia miaka minne tangu mwaka 2011 hadi 2015 limegharimu shilingi bilioni 139.20 za Tanzania lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88. Pia katika jengo hili kuna sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la kuogelea, Sehemu za kufanyia mazoezi, maegesho ya magari na sehemu nyingine muhimu.
Kudumu kwa rekodi ya urefu ya PSPF Towers lenye minara miwili na ukubwa wa mita za mraba 73,000, kutategemea kukamilika kwa majengo mengine yanayochipua kwa kasi katika Afrika. 


Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Majengo haya yanatoa muonekano mzuri wa majengo ya kisasa ya katikati ya mji.

    ReplyDelete
  2. Hiyo minara ya PSPF ina urefu wa mita 147 haiwezekani itajwe ndilo jengo lefu kuliko yote Afrika Mashariki na Kati. Kuna jengo linaitwa UAP Tower lenye ghorofa 33 na urefu wa mita 163 (535 ft). Kwenye ukweli tuseme ukweli tusilazimishe sifa, labda tuishie kusema tu kuwa minara ya PSPF ni jengo lefu kuliko yote Tanzania.

    ReplyDelete
  3. Vipi kuhusu UAP Tower lililoko mjini Nairobi lina urefu wa mita 163 (535 ft)????

    ReplyDelete
  4. Rekodi iliyoandikwa katika ripoti hii inakinzana na rekodi iliyoandikwa katika Wikipedia, kama mdau hapo juu anavyoeleza. Sasa sijui usahihi u wapi?

    ReplyDelete
  5. Tumia akili ya kawaida tu, ghorofa 35 za PPF haziwezi kuzidiwa na 33 za UAP, msilete ubishi wa siasa hata kwenye vitu vidogo kama hv!!!

    ReplyDelete
  6. Wewe unayesema msilete siasa hapa unahitaji kutumia common sense kuliko kukurupuka tu na kutumia nguvu kubwa kubisha. Kwa taarifa yako ghorofa chache zaidi zinaweza kuwa refu kuliko ghorofa nyingi kutegemeaba na aina ya ujengaji na deisign ya jengo.

    ReplyDelete
  7. Times tower Kenya is 35flrs which is shorter than UAP tower in height so the number of flrs don't determine the height of the building.UAP tower remains the tallest building in East Africa just for few months before the completion of britam tower and hazina tower,and of course the undisputed Haas tower which us under construction with 70flr split 45 and 25

    ReplyDelete
  8. Kenya is still the power house of east africa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...