Jukwaa La Sanaa la BASATA wiki hii lilipata wazungumzaji wa aina yake na kulifanya kuwa jukwaa lililochangamka na kuwa na mazungumzo ya zaidi ya masaa matano. Wasanii takriban 70 walikaa wakichambua maada mbalimbali kuhusu mustakhabari wa sanaa katika nchi yetu. Jambo ambalo liliingiza changamoto katika jukwaa hili, ni kuweko katika meza kuu wasanii wawili ambao walianza sanaa nchini na hatimae kuhamia ughaibuni ambako ndiko wanaishi kwa sasa.

Wasanii Salma Moshi aliyekuwa akijulikana kama Salma Nyoka, msanii wa kwanza wa kike kuchezea nyoka katika jukwaa, na ambaye alikuwa kiongozi wa vikundi vilivyotamba kama DDC Kibisa Cultural Troupe Super Mama Cultural Troupe na Ujamaa Cultural Troupe, na Abbu Omar, mwanamuziki aliyewahi kupigia bendi kama Urafiki na UDA Jazz ambae kwanza alihamia Kenya na kupiga na kurekodi na makundi kama Simba wa Nyika na Les Wanyika na pia kurekodi album kadhaa akiwa na kundi lake ambaye hatimae alihamia Japan ambako amekuwa akiishi kwa kupiga muziki na akiwa na waTanzania wengine kama Lista na Fresh Jumbe.

Mazungumzo yaligusia nyanja mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kuwa na mikataba kabla ya kazi, kuboresha kazi ili kuweza kuuza nje, namna ya kujitambulisha  duniani kwa kuwa na websites na blogs, na pia serikali kubadilika na kuweko mfumo wa uongozi wa sanaa kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa. Katika mkutano huo, John Kitime Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki aliongelea fursa ya Bima ya Afya kwa wasanii, ambapo Salma Moshi alijitolea kuwalipia nusu ya ada wasanii wanne, na kumlipia bima kamili Mzee Kassim Mapili ambaye kwa sasa anasumbuliwa na moyo na figo. Abbu Omar pia aliamua kulipia Bima yake na kueleza kuwa katika nchi ya Japan ni lazima kila mwananchi kuwa na Bima ya Afya, kwani ugonjwa hauji kwa taarifa na matibabu ni gharama kubwa.

Mkutano huo ulianza saa tano na kulazimishwa kusimamishwa saa kumi, kwani wasanii bado walikuwa na mengi ya kuwauliza wasanii hawa nguli walioweza kuendeleza maisha ughaibuni kupitia sanaa

Salma Moshi na Mzee Kassim Mapili
Abbu Omari mwanamuziki aishiye Japan akitoa mada. Kulia ni msanii mkongwe aishiye Marekani Salma Moshi aliyepata kujizolea umaarufu kwa kucheza na nyoka miaka ya nyuma
Picha ya pamoja

Salma Moshi akiwa na baadhi ya wasanii aliowalipia sehemu ya Bima ya Afya IMETAYARISHWA NA www.johnkitime.co.tz
Kwa kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...