Na John Gagarini, Chalinze 
HALMASHAURI ya wilaya ya Bagamoyo imeshauriwa kuisitisha mikata ya umiliki wa ardhi iliyochukuliwa na wawawkezaji ambao hawajaiendeleza ardhi hiyo kwa kipindi cha zaidi ya miaka 15 wairejeshe kwenye serikali za vijiji kwa ajili ya matumizi ya umma. 
Hayo yalisemwa na mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete wakati wa mikutano ya hadhara ya kampeni kwenye Vijiji vya Makombe na Kinzagu kwenye kata ya Lugoba na kusema kuwa wamiliki hao kama wameshindwa kuiendeleza ardhi hiyo ni vema wakairudisha kwa wananchi.
 Ridhiwani alisema kuwa inashangaza kuona kuwa wananchi kwenye vijiji hivyo wamekuwa wakihangaika kutafuta ardhi kwa ajili ya kilimo pamoja na matumizi mengine lakini wanakosa maeneo ambayo yamehodhiwa na watu wachache. 
“Kwa sasa ni vema halmashauri zikasitisha mikata ya umiliki wa ardhi hiyo kutokana na kushindwa kuiendeleza kwa kipindi cha miaka zaidi yha 10 ambapo sheria inataka mwekezaji kuiendeleza ardhi ndani ya kipindi cha miezi 32 na endapo atashindwa kuiendeleza anaweza kufutiwa umiliki,” alisema Ridhiwani. 
Alisema kuwa haipendezi kuona wananchi wanahangaika kutafuta maeneo huku baadhi ya watu wakiwa wamehodhi maeneo bila ya kuyaendeleza na kuacha yakiwa mapori ambayo yanahatarisha usalama wao.
 Diwani wa Kata ya Lugoba Rehema Mwene akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Makombe wakati wa mkutano wa kampeni wa kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Makombe wakati wa mkutano wa kampeni wa kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Sehemu ya wakazi wa Kijiji cha Makombe wakati wa mkutano wa kampeni wa kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Msanii Hafsa Kazinja akitumbuiza huku akicheza na mshabiki mbele ya  wakazi wa Kijiji cha Makombe wakati wa mkutano wa kampeni wa kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...