Maelfu ya Wakazi wa Mji wa Kahama na Vitongoji vyake wakimsikiliza  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kujinadi kwa kuwaomba wampigie kura ya ndio asubuhi na mapema Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu,ili aibuke mshindi na kupata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika awamu ya tano.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya Waananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya CCM mjini Kahama jioni ya leo.

Dkt.Magufuli Ijumaa  amefanya mikutano yake ya kampeni  katika wilaya za Mbogwe, Bukombe mkoani Geita  na baadae halmashauri mpya ya Ushetu baadaye mkutano mkubwa wa kampeni  uliofanyika mjini Kahama mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na umati wa watu uliorushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Star TV.

Akizungumza katika mikutano hiyo  wakati akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 25 mwaka huu kumpigia kura za ndiyo, Dkt Magufuli amesema kuwa Serikali yake itashughulikia migogoro ya madereva na kuhakikisha wanapata mikataba kutoka kwa waajiri wao ili kuboresha maslahi yao.
Amesema Madereva ni watu muhimu katika sekta ya usafirishaji na wanafanya kazi ngumu,lakini maslahi yao hayatiliwi maanani,hivyo amesema kuwa atahakikisha yanaboreshwa ili na waone faida ya kazi yao,na iwe yenye kuthaminika ,hivyo serikali ya awamu ya tano itakayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli italifanyia kazi ipaswavyo.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Bukombe mapema Ijumaa mchana, alipokuwa akielekea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa kwa wananchi ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano.
 Mjumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa mji wa Kahama Ijumaa jioni  kwenye mkutano wa kampeni za Urais uliofanyika kwenye viwanja vya CCM mjini humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu. Mh.Sitta a.k.a Mzee wa viwango na kasi pia alimnadi Dkt Magufuli na kumwombea kura kwa wananchi hao za ushindi na hatimaye akaibuke mshindi kwa nafasi ya Rais na kupata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika kipindi cha awamu ya tano.
 Maelfu ya wananchi wa mji wa Kahama wakiwa wamekusanyika mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya CCM mjini Kahama Ijumaa jioni.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwanadi Mgombea Ubunge wa Kahama Ndugu Jumanne Kishimba pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Msalala Ndugu Ezekiel Maige mbele ya maelfu ya wakazi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Wachimbaji wadogo wadogo waishio eneo la Nyarugusu,Wilayani Geita wakimshangilia mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mapema leo jioni alipokuwa akielekea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake.

PICHA NA MICHUZI JR-KAHAMA SHINYANGA

PICHA ZAIDI INGIA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. CCM Songambele ukikata mbuga na kuwika mikoa yote, hoja na sera nzuri tunaendelea kuzisikiliza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...