![]() |
Juma Pinto Mwenyekiti Miss Tanzania |
Mashindano yatakayo fanyika ni ya mikoa tu, hakutakuwa na mashindano katika ngazi ya kitongoji, wilaya wala Kanda.
Sifa za kuwa Wakala wa Miss Tanzania ni pamoja na
1) Uwe na Kampuni iliyosajiliwa na Mamlaka husika ya Serikali.
2) Uwe na mtaji wa kutosha.
3) Uwe na uwezo wa kuandaa shindano katika ufanisi mkubwa.
4) Uwe mstari wa mbele katika kukuza sanaa za utamaduni nchini.
Wakala atakaye pitishwa na Kamati ya Miss Tanzania atapaswa kujisajili Baraza la Sanaa la Taifa.(BASATA) kabla hajapewa kibali cha kuandaa shindano.
Wilaya za Mkoa wa D’salaam, Ilala, Kinodoni na Temeke zitapewa hadhi ya Kimkoa, ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Elimu ya Juu.
Ada ya Uwakala ni shilingi milioni moja(1,000,000/-). Ada ya Uwakala italipwa kwa Kamati ya Miss Tanzania baada ya maombi kukubaliwa na kupitishwa.
Maombi yatumwe kwa barue pepe misstanzania2015@yahoo.com
Kwa mawasiliano na ufafanuzi zaidi piga namba zifuatazo:-
0673 521037 Katibu wa Kamati
0754 337043 Msemaji wa Kamati
0755 019288 Sekretariet.
Imetolewa na:
JUMA PINTO.
MWENYEKITI
KAMATI YA MISS TANZANIA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...