Umoja wa
wanafunzi waliosoma shule ya St Joseph convent school ya jijini Dar es salaam
iliyodumu kuanzia mwaka
1932 hadi 1969 . Na Forodhani Sekondari
ilyokuwapo kati ya 1970 hadi 2008 ( ilipotaifishwa na serikali) na baada
ya hapo St Joseph Cathedral High school 2009 (baada ya kurudishwa kwa kanisa Katoliki)
hadi leo, tumeungana na kuitwa
St. Joseph & Forodhani ALUMNI
.
St Joseph
&Forodhani ALUMNI imeandaa “reunion” mkutano wa pamoja siku ya Jumamosi
tarehe 26 September kwa wanafunzi wote waliosoma shule hizo tajwa hapo juu bila
kujali umri, jinsi, dini au kabila.
Habari
njema, kuna
wanafunzi waliosoma shule hii maarufu, wanaoishi nje ya nchi, wanaotoka Canada,
Australia, New Zealand Uingereza na Seychelles wanahudhuria mkutano huu wa
kishitoria. Kuna wengine
hawajafika Tanzania kwa miaka zaidi ya 30.
Wanarudi kuona shule iliowalea.
Jumamosi tarehe 26 September 2015
kuanzia saa 3 asubuhi kwa shughuli mbali mbali hadi saa 7 mchana katika viwanja
vya St Joseph Cathedral High School.
Katika watu maarufu
wanaotoka nchi za nje atakuwapo Jaji Mkuu wa mahakama ya Rufaa Seychelles ambae alisoma hapo na kumaliza kidato cha nne
mwaka 1968, na baada ya hapo, kuhamia Seychelles na wazazi wake alipo kuendelea na masomo ya juu.
Richard Rugimbana Sr Theodora Faustine
Mwenyekiti wa kamati Mkuu
wa Shule
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...