Na John Gagarini, Mandela 
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete amesema kuwa endapo atafanikiwa kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo atahakikisha zahanati inajengwa kwenye Kijiji cha Kibaoni ili kuwaondolea adha wananchi wa kijiji hicho. 
Aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kijijini hapo kata ya Mandela na kusema kuwa ilani ya chama anasema kila kijiji lazima kiwe na zahanati huku kila kata ikitakiwa kuwa na kituo cha afya ili kurahishisha upatikanaji wa huduma za afya karibu. Ridhiwani alisema kuwa hicho kitakuwa moja ya vipaumbele vyake ambavyo atahakikisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano ujenzi huo unakamilika na wanakijiji wanapata huduma za afya karibu tofauti na sasa ambapo huwalazimu kwenda kijiji jirani cha Mandela. 
“Ilani ya chama inasema kuwa kila kijiji lazima kiwe na zahanati hivyo endapo nikichaguliwa kwenye nafasi hii ya ubunge kwa kushirikiana na wananchi hivyo nitahakikisha zahanati inajengwa ili huduma zipatikane karibu,” alisema Ridhiwani. 
Alisema kuwa hata kata ya Mandela haina Kituo cha afya ambapo kata hiyo ni mpya ambayo imezaliwa kutoka kata ya Miono na kutaka ujenzi wa kituo hicho cha afya kujengwa kwenye kijiji hicho.
 “Katika kipindi cha uongozi wangu wa mwaka mmoja na miezi miwili tumeweza kukarabati zahanati 24 huku nane zikiwa zimejengwa pia tumeweza kufanikisha kujngwa nyumba za waganga pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba na dawa,” alisema Ridhiwani. 
Aidha alisema kuwa bado kuna changamoto ya baadhi ya vijiji kukosa zahanati hata hivyo mikakati ni kuhakikisha zinajengwa ambapo mipango inaendelea kwa kushirikiana na wananchi.
Mgombea Ubunge jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete akibadillishana mawazo na mjumbe wa kampeni Taifa Makongoro Nyerere wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kata ya Miono wilayani bagamoyo mkoani Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. makongorooo...mzee wa kuwasema mafisadi hadharani...makongoroooo...ha ha ha ha kweli bongo tambarare

    mdau texas

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...