

Na wapigwe tu maana hamna namna nyingine..' Mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda akizungumza na akinamama wa UWT Mkoa wa Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa ameweka kando msimamo aliyokuwa nao awali na kuanza kumnadi kwa nguvu mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli huku akiahidi atafanya hivyo nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na shuka hadi shuka.
Kimbisa alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma alipokuwa kwenye mkutano na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) walipokuwa wakizungumza na mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu katika ukumbi wa NEC Makao Makuu ya Chama hicho mjini Dodoma.
Tukio la Kimbisa kumnadi mgombea urais wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea mwenza Bi. Suluhu linaonesha tayari kimbisa amefunga ukurasa wa kutokubaliana ambao aliuonesha mapema mjini hapo wakati wa mchakato wa chama hicho kutafuta mgombea mmoja wa urais atakaye peperusha bendera ya CCM.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...