Wasanii wenye vipaji vya kuimba wakihakiki majina yao kwa DJ Haazu, wa Radio 5 wakati wa mchakato wa RADIO 5 KAMATA KIPAJI uliofanyika katika viwanja vya TP SINZA Jijini Dar es salaam Septemba 12, 2015.wenye lengo la kusaka vijana wenye vipaji na kuwainua kutokana na vipaji vyao.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
Katika kuonyesha kuwa wapo karibu na vijana wa kitanzania katika kuwasaidia kuwainua kiuchumi na kiuwezo,kituo cha Radio maarufu kutoka kaskazini mwa Tanzania ARUSHA Radio 5 kimenzisha mchato maalum wa kusaka vipaji kwa vijana wa kitanzania mchakato ambao umeanzia Jijini Dar es salaam ukiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanamuwezesha kijana mwenye kipaji kufikia malengo na ndoto zake
DJ Haazu akiwajibika.
Radio 5 imekuwa na michakato mbalimbali ili kusaidia vijana katika secta tofauti tofauti zinazohusu maisha yao ya kiuchumi huku ikiwa inawaunga mkono vijana wenye shughuli mbalimbali ambao hufika radioni hapo kuomba saport ikiwa ni pamoja na vijana wa sarakasi,ujasiriamali na fani nyingine.
Mchakato ambao sasa unatajwa kuwa utakuwa msaada mkubwa kwa vijana ambao umezinduliwa Jijini Dar es salaam na kupewa jina la RADIO 5 KAMATA KIPAJI katika viwanja vya TP sinza darajani ilishughudiwa vijana wengi wakijitokeza kuonyesha vipaji vyao ili waweze kuibuka na zawadi mbalimbali ambazo zinatolewa na waandaji hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...