Ndugu Zangu Wana-DMV,
Napenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha kwamba tarehe
14/9/2015, niliteuliwa rasmi kuwa makamu mwenyekiti wa African Affairs
Advisory Group (AAAG) iliyopo chini ya serikali ya kata ya Montgomery,
Maryland (Montgomery County).
Nafasi hii inausika na nyanja zote za maswala ya wahamiaji toka
barani Afrika hususani; elimu,uchumi,uhamiaji, afya, tamaduni, bajeti,sera
na miswada itakayoboresha huduma za jamii kwa Waafrika.
Kutokana na majukumu haya, nimejiuzulu katika nafasi ya makamu
wa rais wa jumuiya ya Watanzania Washington DC, Maryland na Virginia
(DMV), nikiwa na imani kwamba nafasi hii itaniruhusu kuendeleza utumishi
kwa jamii kwa kiwango kitakachowezesha na kuboresha ufumbuzi wa
changamoto zetu hapa ugenini.
Ndugu zangu, naomba mupokee shukrani zangu za dhati kwa
ushirikiano wenu, upendo na kwa kunidhamini na nafasi nyeti ya makamu
mwenyekiti DMV.
Nafasi hii imenipa uelewa wa kina kuhusu changamoto za
wana-Diaspora na mapungufu yaliyomo katika jamii zetu, ambayo yanahitaji
mikakati itakayopelekea kupunguza vikwazo vya maendeleo yetu hapa
ugenini.
Mwisho niwashukurini tena na kuwakaribisha rasmi katika mikutano
ya hadhara ya African Affairs Advisory Group, inayofanyika kila Alhamisi ya
pili ya mwezi, kuanzia saa moja hadi saa mbili usiku (7:00pm- 8:00pm)
Anwani;
1 Veterans Pl,
Silver Spring,
MD. 20910- Civic Center.
Asanteni sana,
Harriet Shangarai
Harriet Shangarai
Nipo Nanyi Daima!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...