

Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika nane sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani.
Nimajonzi
sana kwetu hasa ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda
mimba wako Mroki Mroki 'Father Kidevu' alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga
ndoa Mroki.
Unakumbukwa
na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni
Mke wako Mary O Nathan pamoja na watoto wako wote, wajukuu wako na vitukuu.
Wananchi na majirani
zako wa pale Kijiji cha Kinyenze,Kata na Tarafa
ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakukumbuka sana na kukuombea kila lililo jema katika mapumziko yako.
Tunakumbuka
maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa TUPENDANE,
TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE, baba hakika hili linatendeka na tupo na
umoja uliotujengea na tunajivunia hilo daima.
Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufuata kama tulivyo kufuata hapa duniani.
Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...