Na Woinde Shizza,Arusha.
LISHE duni kwa kinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano imekua chanzo cha vifo vya watoto wadogo pamoja na kinamama hao hali ambayo  hali ambayo inazorotesha maendeleo ya kiafya na kitaaluma hivyo watanzania wametakiwa kutumia lishe bora yenye vitamin na virutubisho ili kujenga jamii yenye afya bora kwa ustawi wa nchi.

Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa Afya Dokta Kebwe S.Kebwe akitoa takwimu za vifo vya watoto na kinamama vinavyosababishwa na lishe duni amewataka kinamama kuzingatia lishe bora hasa katika kabla ya ujauzito na baada ya kujifungua katika siku 1000 za kuzaliwa kwa mtoto ili aweze kukua vizuri kiafya  hususan afya ya akili na kufaulu kitaaluma.


Kebwe amesema kuwa Mtoto aliyezaliwa na uzito pungufu (chini ya kilo 2.5) ana uwezekano wa kufa katika mwezi wa kwanza baada ya kuzaliwa, mara nne kuliko mtoto aliyezaliwa na uzito wa wastani au zaidi.Mtoto mwenye uzito mdogo sana ana uwezekano wa kufa kutokana na ugonjwa wa kuambukizwa mara nane kuliko mtoto aliye na hali nzuri ya lishe.


“Lishe duni inahatarisha maisha ya watoto wa Tanzania kama ilivyo katika nchi zinazoendelea.Tafiti zinaonyesha kuwa upo uhusiano mkubwa kati ya kiwango cha udumavu na vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka 5, katika ngazi ya mikoa nchini” Kebwe

Naibu Waziri wa Afya Dokta Kebwe S.Kebwe amesema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa Masuala ya Lishe ulioandaliwa na Taasisi ya GAIN (Global Alliance for Improved Nutrition)  unaondelea jijini Arusha huku akiwaagiza maafisa afya walioko katika Halmashauri kufanya kazi zao za kuwaelimisha wananchi na kuwashauri juu ya masuala ya lishe badala ya kupangiwa majukumu mengine na Wakurugenzi wa Halmashauri.

Kusoma zaidi bofya HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...