Wananchi wa Mji wa Singida wakiishangilia Chopa ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati ikiwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye wakiwapungua wananchi wa mji wa Singida, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu akimuonyesha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, mfano wa funguo wenye ujumbe, aliopewa na wananchi wa Singida, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akionyesha mfano wa funguo kwa umati wa wananchi wa Singida, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015. 
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.

KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hapo kabla sikuwahi kufikiri kuwa wapinzani hasa CHADEMA wanaweza kuongea vitu ambavyo si vya kweli na ambavyo hawakuwa na uhakika navyo kama suala la Richmond. Nimeamini walipotosha wananchi na wananchi tukapotoka. Sasa sijui vilivyobaki ambavyo navyo waliviongea kama vina ukweli ndani yake au kama wanauhakika au navyo vitageuka kuwa kama Richmond. Kwa hili nashanga siasa. Kinachosemwa huwa kinaushahidi au ni siasa ambazo ni dynamic game.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...