
Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini (TFF) kilichofanyika Septemba 06, mwaka huu kilifanya mabadiliko
madogo ya kamati zake ndogo ndogo.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Blassy Kiondo aliyekua Mwenyekiti wa
Kamati ya Soka la Wanawake ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Soka
la Ufukweni na Sakafuni (Beach Soccer and Futsal).
Amina Karuma ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha
Wanawake nchini (TWFA) na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji aliteuliwa kuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...