Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.), akizungumza na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, kuhusu nafasi na majukumu yao katika uchaguzi mkuu ujao, pamoja na jinsi Serikali ilivyojipanga kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani, huru na haki kwa vyama vyote.
Waheshimiwa Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini,wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb), wakati wa mkutano huo uliofanyika leo 10-09-2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIC) jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...