DAKTARI DHAMANA KANDA YA UNGUJA DAKTARI FADHIL RAMADHAN AKITOA MAELEKEZO KWA
MADAKTARI BINGWA KABLA YA KUANZA ZOEZI
LA MATIBABU KATIKA KIJIJI CHA KITOPE.
DAKTARI FEI JIE AKIMPIMA MTOTO SARA SHAABAN
MARADHI YA MENO NA KOO MKAZI WA KITOPE WILAYA YA KASKAZIN B”.
PICHA NA ABDALLA OMAR - MAELEZO ZANZIBAR.
Mwashungi
Tahir- Maelezo Zanzibar 14/09/2015
Jumla ya
madaktari bingwa tisa kutoka nchini China Medical team wako Zanzibar kwa ajili
ya kutoa huduma kila sehemu mbalimbali
hapa vijijini kwa ajili ya kuwarahisishia wananchi kupata huduma ili waweze kuelewa kujua afya
zao.
Hayo
yamesemwa na daktari Dhamana wa kanda ya
Unguja DR Fadhil Mohammed Abdullah huko katika shehia ya Kaskazini B Kitope
wakati wa zoezi hilo huko kijijini hapo.
Amesema
lengo la madaktari hao kutoa huduma hiyo vijijini ni kuweza kuwarahisishia
wananchi wa vijijini kuweza kupima na kujua afya zao ambapo zoezi hili hufanyika
kila baada ya miezi mitatu na hutolewa bure.
Pia
amesema
madaktari hao wapo nchini wakishirikiana na madaktari wa wizara ya Afya
kwa kutoa huduma hizo huko kijijini na wanachi kuweza kujitambua afya
zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...