
Akitoa
hotuba yake katika moja ya mikutano yake alioufanya katika mji wa
Kibaigwa Dk. John Pombe Magufuli amesema hakuna kitu kinachomuumiza kama
mauaji ya wakulima na wafugaji yanayotokea kati ya wilaya za Kongwa
Mkoani Dodoma na Kiteto mkoani Manyara.
Dkt
Magufuli ameahidi kuwa mara baada ya kuchaguliwa na kuunda Serikali
yake,jambo hilo atalipa uzito wa juu na kulifanyia kazi kwa umakini
mkubwa. “Yaani Mimi Magufuli Nimteuwe Waziri na watendaji wengine wa
serikali halafu Mauaji yatokee watu wafe, Mkuu wa mkoa yupo , Mkuu wa
wilaya yupo na Kamanda wa Polisi yupo wabaki wanapunga upepo, wamiliki
wa Ng’ombe wabaki wanakula maisha haiwezekani,nitalala nao mbele
na Ng’ombe wataliwa msibani kwa uzembe waliousababisha”,alisema
Magufuli kwa msisitizo mkubwa.
Magufuli
amewataka wafugaji na wakulima kuishi kwa amani bila kubaguana, lakini
pia akasema atatumia sheria za ardhi na kuhakikisha maeneo ya wafugaji
na wakulima yanatengwa, ili wafanye shughuli zao na kukuza kipato na
uchumi wao bila kusumbuliwa.
Baadhi
ya wananchi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake wakimsiiliza Dkt
Magufuli alipokuwa akinadi sera zake za kuomba kura ili kushika nafasi ya Urais ya awamu ya tano.
Waziri
Mkuu wa zamani, Jaji mstaafu Joseph Warioba, akimnadi Dkt.Magufuli ambapo alimfagilia kwa kuhubiri amani katika mikutano yake ya
kampeni kuliko,na pia amewaasa vijana kuilinda amani ya nchi iliopo kwa gharama yoyote,kuishi bila kubaguana.
Dkt.
Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa Dodoma Mjini,mara baada ya
kumkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Ndugu Anthony Mavunde wakati wa
mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri mjni Dodoma leo.
Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje,mjini MPwapwa katika uwanja wa mgambo.
Mgombea
urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimnadi Mgombea ubunge
Jimbo la Kongwa, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati wa mkutano wa
kampeni jimboni humo.
Mawaziri wakuu wa zamani, John Samuel Malecela na Jaji Mstaafu Joseph
Sinde Warioba wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli alipokuwa
akiwahutubia wananchi wa Dodoma kwenye mkutano wa kampeni.
Dk Magufuli akijipigia kampeni kwa wakazi wa Kibaigwa , wilayani Kongwa leo.Akiwa
wilayani Kongwa, Dk Magufuli amesema kuwa akishinda urais atahakikisha
anadhibiti mapigano kati ya wakulima na wafugaji yanayoendelea nchini
na kusababisha vifo vya watu wengi
Dkt. Magufuli akiwapungia mikono wananchi alipowasili kwenye kampeni Uwanja wa Jamhuri Dodoma leo.
Magufuli semaa
ReplyDeleteSemaa usiogope semaaa
Magufuli sema
Sema usiogope semaa
Sisi vijana.......
Wiki ya mwisho ya Oktoba watasoma namba CCM mbele kwa mbele
ReplyDelete