Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo
la Makambako Ndugu Deo Sanga wakiwaiambisha wananchi wa Mafinga katika
uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa Jumapili Septemba 27 kwenye
mkutano wa hadhara wa kampeni.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mafinga
katika uwanja wa Mafinga mkoani Iringa Jumapili Septemba 27 kwenye mkutano wa
hadhara wa kampeni.
Mmoj
wa Waangalizi wa Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka
huu,akifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli
mjini Makambako jioni ya Jumapili Septemba 27 mkoani Iringa
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Ndugu Mahmoud Mgimwa akipiga push up
mbele ya wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa
kampeni wa kumnadi mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
ambaye anashuhudia tukio hilo katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja
vyaWambi mjini Mafinga mkoani Iringa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa
wananchi.
Dk.
John Pombe Magufuli amewaambia wakazi hao wasihadaike na maneno ya
kisiasa yanayotolewa na vyama vingine kuwa nchi ya Tanzania haijapiga
hatua ikiwa chini ya utawala wa CCM wakati maendeleo yanaonekana wazi na
nchi inazidi kusonga mbele kwa mambo mengi ikiwemo amani na utulivu wa
nchi.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa
Chimala,Mbarali mkoani Mbeya alipokuwa akielekea mkoani Iringa kuendelea
na kampeni zake.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe
Magufuli akionesha hisia zake mara baada ya kuonana uso kwa uso na Waziri Mkuu Mstaafu na Kada Mkongwe wa chama cha CCM. Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya
kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe
Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu na Kada Mkongwe wa chama cha CCM, Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa
kampeni,huku Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Ndugu Bulembo akifuatilia kwa
makini
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Rujewa
mjini katika viwanja vya Barafu mjini Rujewa,wilaya ya Mbarali mkoani
Mbeya Jumapili Septemba 27 kwenye mkutano hadhara wa kampeni.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa
Rujewa mjini wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya Jumapili Septemba 27 kwenye
mkutano hadhara wa kampeni.
PICHA NA MICHUZI JR-IRINGA
PICHA ZAIDI INGIA HAPA
PICHA NA MICHUZI JR-IRINGA
PICHA ZAIDI INGIA HAPA
ANKAL
ReplyDeleteKwa sisi tulio nje ya nchi wakati huu na tuna kiu kikubwa mno kujua maendeleo ya kampaini huko bungo, twafika mara tano na zaidi kwenye blog kujisomea maendeleo.Hala hala usije ukatusahau.