Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Huyu yeye ndiyo anayetaka kuwagawa waTZ kwa udini, naweza kupata ujumbe wake kuwa waisilamu wasiwakubali ukawa, ni tamko la kisiasa sana ni sidhani kama ni msemaji wa dini ya kiisilamu.

    ReplyDelete
  2. Nianze na hili la ndoto ya Gwajima akiwaona masheikh mbio mbio wakikimbilia neno la bwana na madrasa zikigeuzwa kua chekechea....hii ni ndoto ambayo bwana Gwajima ameota....wataalamu wa masuala ya ndoto wanatuambia kwamba kwa kuzingatia nyakati ndoto zimegawanywa ktk makundi mawili, ndoto za usiku na ndoto za mchana, hizi za usiku pia zimenyambuliwa na kuelezewa kwamba kuna za usiku mnene na usiku mwepesi ulio karibu na mapambazuko.Tafsiri ya ndoto na maana inategemea mnyambuliko wa nyakati hizo.Wataalamu wa ndoto wakaturahisishia tafsiri na maana za ndoto kwa kutuambia kwamba mara nyingi ndoto zinazootwa usiku mwepesi na zile zinazootwa ktk mwangaza wa jua hazina ukweli na ni za kishetani.Sina hakika huyu bwana aliyeota aliota wakati gani na kwakua hajasema wakati alioota ndoto yake hivyo sioni mantiki ya kuwajengea hofu watu kwa vitu visivyokua na uhakika.Ivi kweli ndoto ya Gwajima imewatia hofu na kuwanyima raha wanawazuoni waliobobea? Kitabu kitukufu kinaelezea ndoto ubora wake,uhalisia wake, usafi wa muotaji nakadhalika hivyo kuna vitu vingi tu vya msingi vinavyopaswa kuzingatiwa ili ndoto iaminike siamini hata kidogo kwamba huyu muotaji ndoto yake yaweza leta athari kwa umma, hata kidogo na wala si kitu cha kukizungumzia ni cha kukipuuza na sababu ya kusema hivyo ni uhakika nilio nao kwamba muotaji hajakidhi vipengere vya ndoto za kweli nilivyovitaja hapo juu.Hili la Mheshimiwa Lowassa sina hakika kama anaweza kusema yaliyosemwa kama nukuu, sina shaka kwamba yeye ni kiongozi wa umma na tunamjua vizuri na amepita sehemu zote kushoto na kulia ktk kujitambulisha hatukuona tatizo lolote. Wagombea uraisi wapo wengi sasa iweje kuhusu mahakama maalum aulizwe mtu mmoja?? awa wengine vp????Namalizia kwa kusema ni vizuri kutafakari kabla hujatoka hadharani na kuzungumza kwa sauti kubwa na hasa kama ujumbe haujakamilika.Nahisi kama kuna maslahi ya kundi,watu, upande flani walioamua kutumia mtu fulani mwenye muonekano sawa na watu fulani ili ionekane anawawakilisha watu fulani.Haipendezi zaidi ni kujidharirisha kwakua vigezo ni vyepesi mnooooooo kuleta ushawishi.

    ReplyDelete
  3. Gwajima ni tishio kwa Amani ya Tanzania. Ameyasema hayo ya kugeuza misikiti kuwa Sunday Schools ndani ya kanisa lake na amekuwa-recorded kwa video. Ndio mshenga wa Lowassa. Nafikiri waislamu wote bila kuogopa na kubabaishwa na ulaghai ni kutowapa nafasi kabisa Lowassa na Gwajima wake, ni kura ya HAPANA kwa Lowassa. Hawatufai kabisa, Kwanini hii Chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu? Hasaa huyu Gwajima mshenga wa Lowassa.

    ReplyDelete
  4. Kama serikali ikiruhusu matamko kama haya yatolewe na kupewa nagasi ktk vyombo vya habari hapo ndipo matatizo yanapoanzia kuliko maneno yaliyosemwa ktk ndoto ambayo wengi hawakuyasikia. Ni wazi msemaji anawakilisha upande mmoja ktk siasa zetu.

    ReplyDelete
  5. Ukizingatia maneno ya Lowassa na Gwajima,dahahiri no dharau kwa Waislam wa nchi.Lowassa asipoangalia mambo Haya ya udini yanaweza kumgharimu ktk uchaguzi.Ni vizuri akamdhibiti mahabuba wake Gwajima asije akamharibia.Waislam tumamkumbusha yaliyo mkuta Mrema mwaka 1995.

    ReplyDelete
  6. Tatizo sio ndoto ya Gwajima kama mtu tu wa kawaida, tatizo ni ndoto Gwajima kama mtu ambae amejanasabsha na UNABII au UTUME kama ambavyo anavyojiita na ambavyo anaonekana na wafuasi wake. Kumbukeni kuwa Gwajima ana kundi kubwa la watu wanaomfuata nyuma yake hivyo basi kitendo chake cha kusema hayo aliyoyasema hakiwezi kunyamaziwa kimya kwa sababu tuna mifano hai ya machafuko au fujo zilizoanzia na mafunzo au mafundisho ya makanisa kama haya ya kina Gwajima. Mfano mdogo tu ni kitendo cha Kijana aliyeikojolea Quran ambayo ni kitabu kitakatifu cha Waislam halafu mama yake nae akatoa maneno ya kukibeza kitabu hicho na kuwabeza waislamu. Nadhani bado kumbu kumbu imo kichwani ya kilichotokea baada ya hapo. Hayo ni matokeo ya kauli kama hizi za kina Gwajima na hazipaswi kunyamaziwa wala kufumbiwa macho.

    Pili kitendo cha Lowasa kudai rais lazima mwaka huu awe Mlutheri, basi itafika mahali nako Waislamu wa madhehebu mengine wataanza nao kudai Rais wa dhehebu la Answar Sunna, Shia, Bohora, Ismailia na kadhalika. Na wakristo wengine nao waanze kudai rais wa madhehebu mengine, na Wapagani nao wadai kutoa rais na Mabudha, na wengineo. Tufke mahali tukemee kauli za aina hiyo ni za kipuuzi kabisa na hazina nafasi kwenye jamii yetu. Na siwezi kushangazwa na kauli hiyo ya Lowasa kama mshauri wake ni huyo Gwajima anaetoa kauli zisizo na mashiko.

    SHeikh Khalifa huwa hapepesi macho wala hajipendeki kwenye kusema ukweli,tunatambua harakati zako tangu enzi za Sheikh Kassim Bin Juma na tutakuunga mkono kwa hili kwa kuisambaza hii taarifa kwa waislamu wengine kwa sababu hii nchi ni yetu sote sio ya dini moja au dhehebu moja.

    ReplyDelete
  7. Verbal diarrhoea
    There was no need of rumbling over an overtly dangerous political mistake. You dont mix religion with politics where you are aiming at establishing a form of democracy. Kama wamevunja sheria kuna mahakama nchini. Full stop.

    ReplyDelete
  8. Ubaguzi wa kidini au kikabila au kiasili au ki rangi ni kosa la kimaadili tuu. Ubaguzi hapa tz si kosa zito kama yalivyo ya jinai na ndo maana hakuna sheria wala adhabu kwa wabaguzi. Ubaguzi ungekuwa mbaya kama wizi au uuaji basi ungeona ingekuwa jinai na ingewekwa kwenye criminal procedure na penal code (kanuni za adhabu).

    Sijaona kama Lowasa kafanya kosa la jinai na kustahili adhabu yoyote. Na gwajima ana haki ya kuota ndoto aitakayo kama mwakipesile. Ana haki ya kuendeleza dini yake na kutamani watu woote wangefata. Na hii ni haki walionayo masheikh ya kutamani maaskofu wangekuwa wafuasi wao.

    pia kuna suala la free speech, wote, lowas, gwajima, na msemaji wa video wana haki na uhuru wa kueleza wanachodhani. kukubaliana nao na kuwakataa pia ni sehemu ya uhuru wa kauli. msiwasulubu kwa uhuru wenu wa kauli.

    Mkitaka ubaguzi uwe kosa zito basi katiba mpya iweke mpango mzuri wa kushughulikia ubaguzi kama jinai. Nchi kama USA wanafanya hivyo. Kazi ikitangazwa basi nyaraka za maombi zote huhifadhiwa kama ushahidi wa kuonyesha kuwa aliyeajiriwa ndiye bora ya waombaji woote. Tz mwombaji anayeajiriwa anaweza kuwa aliyefeli na wasiajiriwa ndo hasa wataalam. hatutaendelea kama ubaguzi utaendelea kuwa kosa dogo. na jinsi muda unavyosonga mbele ndo ubaguzi huo utazidi kukomaa maana sasa hivi bado ni wa siri.

    ReplyDelete
  9. Kweli kweli mnatiwa hofu na Gwajima hadi mtoe press conference kumuhusu? Kama kuna maneno mgombea Lowasa ameyasema, sawa, tuyajadiri lakini ya hizi ndoto za huyu kilaza anayejiita askofu kweli si za kutufanya tupoteze mwelekeo unaohitajika na watanzania. Mabadiriko natumai mnayataka pia au kama kweli mnaamini kuwa Sunday schools ... Basi, tuichague CCM kwani hawana hii idea lakini maisha yetu yabaki palepale.

    ReplyDelete
  10. Gwajima kweli amekosea ila kitendo cha kurudia tena alichokosea na kukizungumza hadharani ni sawa na kukimwagia Petrol mbele ya jamii na wote Gwajima na Imam Bukhary wote mnachangia kuivunja Amani!

    Wote kuweni makini na mngefuata channel husika na Sio kurudia mada ambayo Watanzania wengi hawakuisikia; Editors wa Vyombo vya habari Msiwape nafasi ata kidogo watu kama Gwajima wala Imam Bukhary maana wote hawapimi maamuzi yao.

    Asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...