Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wake wa kampeni  uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Kalangalala mjini Geita jana  na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Mgombea Urais Huyo amewaambia wananchi wa Geita kuwa mara atakapoingia Ikulu, moja ya changamoto anazotarajiwa kuzipa kipaumbele ni pamoja na suala la kutatua mgogoro wa wachimbaji madini wadogo wadogo.
Magufuli ameasema kuwa akiingia madarakani atawapa maeneo wachimbaji wadogo wa madini nchini ikiwa ni pamoja na kuwakopesha mitaji na kuwapa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi zao pamoja na mafunzo kwa ajili ya  kuboresha uchimabaji wao ili uwe wa kisasa zaidi na kupandisha  kiwango cha  ufanisi wa kazi zao za uchimbaji.

Dkt. Magufuli leo amehutubia mikutano katika miji ya Runzewe wilayani Bukombe, Katoro wilayani Chato na Geita mjini akiendelea na kampeni zake za kwaomba wananchi kumpa kura za ndiyo ili aweze kuingia Ikulu na kuwafanyia kazi Watanzania kama kiongozi na Amiri Jeshi mkuu wa Tanzania. 
Wananchi wa mji wa Geita na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Kalangalala,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kumwaga sera zake mbele za wananchi hao ikiwemo pia na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais kwa kushinda kura nyingi ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwandani Wagombea Ubunge wa jimbo la Busanda Mh.Lolensia Bukwimba na Dkt Meedad wa Chato mapema mchana huu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,katika mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.Dkt Magufuli atahutubia jioni ya leo mjini Geita kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita mapema leo mchana kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.
 Wananchi wa Runzewe wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa kampeni.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita na mgombea ubunge wa jimbo la Geita vijijini Ndugu Joseph Kasheku a.k.a King Msukuma akihutubia malefu ya wananchi wa Geita mjini kwenye mkutano wa kampeni wa Urais,ambapo Ndugu Joseph aliwaomba wakazi wa Geita na vitongoji vyake kumchagua Dkt John Pombe Magufuli awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka. 
Magufuli Style ilitikisa pia ndani ya Geita kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt John Pombe Magufuli ambapo wasanii walipasha kwanza kabla ya kuanza kazi.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwapokea  mlemavu wa ngozi Albino Lazaro Malendeka kushoto ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Brigade cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita  na William Mabula Msalaba aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Geita.
 Wananchi wa Katoro wakiushangilia msafara wa Dkt Magufuli alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...