Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda(wa pili kulia)kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi za Idd el Hajj Meneja wa Mahabusu ya Watoto mkoa wa Arusha,Mussa Mapua leo kwa ajili ya kusherekea siku kuu hiyo leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete ametoa zawadi mbalimbali katika Mahabusu ya watoto walikinzana na sheria iliyopo jijini Arusha
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Kikwete,Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda amesema pamoja na kuwa watoto hao wanakabiliwa na mashtaka ya kujibu lakini mheshimiwa Rais anatambua haki zao za kushiriki na jamii kufurahia siku kuu hiyo ya kidini.
"Kama mnavyofahamu Rais Kikwete amekua na utamaduni wa kuwakumbuka katika siku kama hizi ili nanyi mfurahie siku kuu hii,"alisema Mapunda.
Akipokea zawadi hizo Meneja wa Mahabusu hiyo,Mussa Mapua amesema imekua ni faraja kwa kiongozi wa nchi kuwakumbuka na kuomba taasisi nyingine na watu binafsi kuiga mfano huo na kumtakia Rais Kikwete mapumziko mema anapojiandaa kumaliza muhula wa pili wa uongozi wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...