Na Mwene Said wa
Blogu ya Jamii

Kulia ni msanii wa Nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha (32) aliyekuwa anakabiliwa na mashitaka ya ubakaji leo  aliachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, baada ya ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo. 
 Mbasha ambaye pia ni mume wa msanii wa nyimbo za injili nchini, Flora Mbasha, alipiga magoti na kuangua kilio nje ya mahakama baada ya kusomwa hukumu hiyo iliyomwachia huru dhidi ya tuhuma za ubakaji. 
Hukumu hiyo ilisomwa jana saa 4:45 hadi saa 5:15 asubuhi na Hakimu Mkazi Flora Mgaya wa mahakama hiyo. 
 Hakimu alisema baada ya ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa Jamhuri na ushahidi wa mshtakiwa, mahakama imeona bila kuacha shaka hautoshelezi kumtia hatiani. 
 Alisema mahakama yake inamwachia huru mshtakiwa Mbasha. Mbasha alitoka kasi kwenye chumba cha mahakama na kupiga magoti huku akili kwa sauti na kusema ‘Mungu amenitetea katika maisha yangu… Mungu amenilinda, ameniepusha na kwenda kuozea jela … namshukuru sana sina cha kumlipa’ alisisitiza wakati akilia mahakamani hapo.
 “Mniache sina kitu cha kuongea Mungu wangu yu hai amenitetea na kuniepusha na kuozea jela mimi…” alisema Mbasha huku akilia na kuzungukwa na watu pamoja na wanahabari. 
 Katika kesi ya msingi, ilidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa). 
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa). Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo na alikuwa nje kwa dhamana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Majeshi ya Shetani Yameshindwaaaa.Uhimidiwe Mungu uliyeumba Mbingu na nchi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. MUNGU hawezi kumtupa mja wake,yuko wapi MUNGU wa flora?hakika MUNGU wa mbasha yu hai,naungana NA mbasha kumtukuza MUNGU kwa kumtetea mja wake,AMINA KUBWA.

      Delete
  2. ACHANA NAE KABISA HUYO FLORA SI MTU MZURI KWAKO. TAFUTA MKE MWINGINE WA KUOA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...