Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kila chama kifanye  kampeni za kistaarabu ili kila mtu aende Ikulu  pasipo kuvuruga amani.

Mbowe ameyasema hayo leo mbele ya waandishi wa habari wakati wa kuelezea masuala ya kampeni zinazoendelea kwa vyama vyote vya siasa, pia amesema kuwa kuna kauli za viongozi wa baadhi ya vyama ambazo haziridhishi katika kupiga kwao kampeni.

Mbowe amasema kauli ya watu hao ni ya kichochezi na haiwezi kuvumilika lakini chama husika hakikuweza kufuta kauli hiyo.

Aidha amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekaa kimya kwa kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya vyama kuwa hawawezi kuachia watu wakatawale Ikulu.

Amesema kumekuwa na changamoto katika umoja wa katiba ya wananchi lakini hadi sasa mgogoro wa majimbo hauzidi 10 ambapo ni hatua nzuri kwa umoja huo nia yao ni kwenda Ikulu na sio kuwagwana majimbo kama sadaka.

Mbowe amesema tatizo la viongozi waandamizi  NCCR-MAGEUZI, inatokana na kutaka majimbo wasimame licha kutambua mtu anapewa kugombea  kutokana na sifa alizonazo  pamoja na uwezo wa mtu kushinda katika uchaguzi mkuu.
 
 Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani)juu hali ya kampeni inayoendelea kwa baadhi ya vyama kushindwa kufanya kampeni za kiistarabu leo Ngome ya UKAWA jijini Dar es Salaam leo,kulia ni Afisa Habari wa Chama hicho,Tumaini Makene.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Freeman Mbowe leo makao makuu ya ngome ya UKAWA jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...