Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM) jimbo la Kibamba Dkt Fenella Mukangara akiongea na wakazi wa eneo hilo
wakati akipokuwa akitangaza sera za chama chake na kuwaomba wampigie kura
katika uchaguzi ujao pamoja na madiwani wengine sita wa chama cha mapinduzi.Dkt
Fenella alitaja vipaumbele vyake katika jimbo hilo ambavyo ni Maji,Elimu,Afya
pamoja na ajira kwa Vijana na kuwasihi wakazi hao kuchagua maendeleo bora
yatayopatikana ndani ya CCM.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bw.Salum Madenge akimnadi Mgombea Ubunge jimbo jipya la kibamba Dkt Fenella Mukangara(waliokaa aliyesuka) kwa
wakazi wa kibamba leo hii jijini Dar es Salaam.Bw Madenge aliwasisitiza wakazi
wa jimbo ilo kumchagua Bi Fenella kwani ni mtu shupavu,mwenye kupenda maendeleo
na mzalendo
Mmoja wa wakazi wa kibamba aliyejitokeza
kumsikiliza Mgombea Ubunge kwa Tiketi ya CCM akiwa amenyanyua bango lenye
ujumbe maalum kumhusu mgombea jijini Dar es Salaam.
Wakazi
wa kibamba waliojitokeza kwa wingi wakimskiliza kwa makini mgombea ubunge jimbo
la kibamba Dkt Fenella Mukangara akinadi sera zake pamoja na
Mgombea uyo kutaja vipaumbele kwa jimbo ilo kuwa ni Maji,Elimu,Afya na ajira
kwa Vijana.
Wakazi
wa kibamba waliojitokeza kwa wingi wakimskiliza kwa makini mgombea ubunge jimbo
la kibamba Dkt Fenella Mukangara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...