Msanii
maarufu nchini Afrika Kusini, K.O akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya ziara ya ktembelea vyombo mbalimbali vya habari hasa Televisheni na Redio na kuangalia mziki wa hapa nchini katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.

Msanii
maarufu nchini Afrika Kusini,K.O (Katikati) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) juu ya ziara yake nchini leo jijini Dar es
Salaam,Kushoto ni Tsholofelo Moremedi wa Cashtime Life Menagement na Kulia Afisa Mtendaji Mkuu wa Cashtime Life, Thabiso Khati.
Waandishi
wa habari wakimsikiliza Msanii K.O juu ya ziara yake nchini katika
ukumbi wa idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya JamiiMSANII
marufu nchini, Afrika Kusini,K.O ametua nchini kwa ziara katika vyombo
vya habari kuona jinsi wanavyoshirikiana na wasanii nchini.
Akizungumza na waandishi habari jijini,K.O amesema ziara hiyo anatarajia kupita katika vyombo vya habari vilivyo nchini na kuona jinsi gani wanavyofanya nano kazi wasanii.
K.O ameingia nchini jana ambapo kazi yake imeanza jana na itaendelea hadi Septemba 16 mwaka huu na kuangalia uwezekano wa kushirikiana na wasanii nchini.
Msanii huyo ameshinda tuzo mbalimbali na ametamba wimbo wa Caracara na ameweza kushirikiana na baadhi ya wasanii nchini akiwemo Vanessa Mdee katika wimbo Nobody but me.
K.O kufanya ziara nchini ni ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na akitoka nchini anaratarajia tena kufanya ziara nchini Kenya pamoja na kufanya onyesho la mziki katika ukumbi wa Ebony Mjini humo.
Amesema Tanzania inakuwa kwa kasi katika sekta ya mziki Afrika na wasanii wana vipaji vinavyoonekana na kufanya waweze kujulikana kimataifa na kuongeza kuwa anatarajia kutengeneza mziki mpya atakao washirikisha wasanii watanzania.
K.O anasimamiwa na Kampuni ya Cashitime Life ya nchini inayojihusisha burdan ambapo kampuni hiyo imeweza kumtangaza ndani ya nchi huyo pamoja na nje.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...