Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al – Hajj Dr. Ali Mohammed Shein amesema ni jambo la faraja kuona kwamba waumini wa Dini ya Kiislamu waliojalaliwa uwezo wanaendelea kujitokeza katika ujenzi wa majengo ya Misikiti na madrasa za Kisasa katika maeneo mbali mbali hapa Nchini.
Alisema mwamko huo umesaidia kupata majengo mazuri nay a kisasa kwa mujibu wa maendeleo ya sayansi na teknolojia kiasi kwamba mazingira ya kufanyia Ibada yanaridhisha katika kuwafundisha vijana Quran n a mafundisho mengine ya Dini ya Kiislamu.
Al-Hajj Dr. Ali Mohammed Shein alisema hayo wakati akizungumza na Waislamu wa mbali mbali mara baada ya kuuzindua rasmi Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Umbuji { Masjid Shuraa } ndani ya Jimbo la Uzini Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Alisema Waislamu na Jamii ni mashahidi katika miaka iliyopita Waislamu wa Zanzibar na maeneo mengine Duniani hawakuwa na sehemu muwafaka wakati walipokuwa wakitaka kutekeleza ibada zao.
Alisema mazingira ya sasa yamekuwa bora zaidi kwa kuwapa utulivu waumini wa Dini ya Kiislamu ambapo hufanya ibada zao katika maeneo mazuri yanayotoa fursa kuendelea na ibada hizo hata wakati wa usiku.
Rais wa Zanzibar alisema ujenzi wa msikiti huo ni neema kubwa ambayo waumini wa Kijiji hicho wana wajibu wa kushukuru na kuhakikisha wanautumia vyema katika kutekeleza ibada za sala, kuendesha madrasa, kukuza imani, kuuendeleza Uislamu na kufanya matukio ya Kijamii ambayo yana mnasaba wa kutumia msiki.
Aliwanasihi waumini hao kuitunza nyumba hiyo ya mwenyezi Muungu kwa kuwaunganisha wakikumbuka kwamba uwepo wa jengo hilo tukufu ujenzi wake umetokana na Umoja na moyo wao wa kujitolea ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya ujenzi.
Akisoma Risala ya Waumini na Wananchi wa Kijiji cha Umbuji Ustadhi Haji Shauri Issa alisema ujenzi wa Msikiti huo wa Ijumaa wa Kijiji hicho ulioanza Miaka Mitatu iliyopita umekuja kutokana na changamoto ya ongezeko kubwa la Waumini waliokuwa wakifanya ibada katika msikiti wa asili.
Ustadhi Shauri alisema waumini wa Kijiji hicho wamepata faraja baada ya kukamilika kwa msikiti huo uliojengwa kwa nguvu za waumini wenyewe na na kuwashukur washirika mbali mbali wa Dini waliojitolea kuchangia ujenzi huo.
Msjid Shuraa ambao una uwezo wa kusaliwa na waumini zaidi ya 600 kwa wakati Mmoja umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 200,000,000/- za Kitanzania licha ya kuendelea kuwepo baadhi ya changamoto katika kukamilisha msikit
Haiba ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Umbuji ulipo Jimbo la Uzinin ndani ya Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja unavyoonekana kwenye picha baada ya kukamilika ujenzi wake na kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohammed Shein.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Umbuji mara baada ya kuuzinduai Msiki wa Ijuma wa Kijiji hicho.
Naibu Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Thabir Nauman Jongo akitoa mawaidha katika hafla ya uzinduzi wa Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Umbuji Jimbo la Uzini ,Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakisikiliza Hotuba ya Balozi Seif mara baada ya uzinduzi wa Msiku wa Ijumaa wa Kijiji hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Balozi Mpya wa India aliyepo Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya aliyefika Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Balozi Mpya wa India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya aliyekaa kati kati katika azma ya kuimarisha uhusiano wa muda mrefu wa Kihistoria kati ya pande hizo mbili. Aliyekaa mwanzo kutoka kushoto ni Balozi Mdogo wa India aliyepo hapa Zanzibar Bwana Setandar Kumar. Picha na OMPR – ZNZ.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...