Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (kushoto), na Afisa wa Fedha Mwandamizi wa Mfuko huo, Angel Mukasa, (kulia), na Mfanyakazi mwingine wa Mfuko huo, Omari Bundile, (wapili kushoto), wakigawa mafuta maalum yanayotumiwa na watu wenye ulemavu wa ngozi, pamoja na sare za shule na viatu kwa wanafunzi hawa wenye ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2015. Katika kutekeleza sera ya mfuko ya kusaidia jamii, PPF, imetoa vifaa mbalimbali ikiwemo, sare za snhule, viatu na mafuta hayo maalum, Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Lulu Mengele aliwaambia waandishi wa habari.
(Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
(Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Latifa Musa,(kulia), akitoa shukrani kjwa niaba ya wenzake baada ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam, kupatiwa msaada na Mfuko wa Pensheni wa PPF
Watoto wenye ulemavu wa ngozi kwenye shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa msaada kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF, shuleni hap oleo Ijumaa Septemba 11, 2015
Watoto wenye ulemavu wa ngozi, wakiteta jambo, baada ya kupatiwa msaada wa vifaa yakiwemo mafuta maalum yanayotumiwa na watu wenye ulemavu wa ngozi

Picha ya pamoja ya maafisa wa PPF, Walimu na wanafunzi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...