Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa Mashine mbili ambazo zitatumika kufuatilia mapigo ya moyo ya mgonjwa mahututi akiwa kwenye tiba ( Patient Cardiac monitors).
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mashine hizo ambazo zimetolewa na Mfuko wa Human Welfare Trust, Veena Joa, amesema wataendelea kusaidia kutoa huduma mbalimbali kwakua Hopsitali ya Taifa Muhimbili inategemewa na wananchi wengi wana imani nayo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dkt. Hussein Kidanto amewashukuru Human Welfare Trust kwa msaada wa mashine hizo ambazo zitatumika katika Kitengo cha magonjwa ya dharura hapa MNH na kueleza kwamba kitengo hicho ni sehemu muhimu kwani kinapokea wagonjwa wengi kabla ya kupelekwa Wodini.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya magonjwa ya dharura na ajali MNH ambaye pia ni Daktari Bingwa wa magonjwa hayo Dkt Juma Mfinanga, kwa siku kitengo hicho hupokea wagonjwa 150 hadi 200 na kati ya hao asilimia 60 hadi 70 wanakuja wakiwa mahututi.
![]() |
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk Juma Mfinanga akipokea moja ya mashine za kufuatilia mapigo ya moyo ya mgonjwa mahututi wakati wakiwa kwenye tiba kwenye hospitali hiyo. |
Baadhi
ya wawakilishi wa mfuko wa Human Welfare Trust wakikabidhi mashine hizo kwa
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji MNH, Hussein Kidanto.
Baadhi
ya wawakilishi wa mfuko wa Human Welfare Trust.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...