Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Covenant, Sabetha Mwambenja,
wapili (kushoto) akimkabidhi gari Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi
Mussa Natty wapili (kulia) kwaajili ya Wanachama wa Taasisi ya Federation
waliojitolea kutoa elimu elimu ya ugonjwa
wa Kipindupindu na kufanya usafi katika Manispaa hiyo (kulia) Mwenyekiti wa
bodi wa Benki hiyo Balozi, Salome Sijaona na Mratibu wa Federation Taifa, Khadija
Kingi.

Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Covenant Balozi, Salome
Sijaona, kwa Pamoja na Mkurugenzi wa Benki hiyo Sabetha Mwambenja(Kushoto)
wakikabidhi vinywaji kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa
Natty, na Mratibu wa Taasisi ya Federation Taifa Khadija Kingi, Ikiwa ni sehemu
ya kuwezesha kampeni ya kupambana na kipindupindu kwa Manispaa hiyo.
Manispaa yazindua mpango wa
kukitokomeza
BENKI ya Covenant imetoa msaada
wa basi maalumu kwa ajili ya kuwasafirisha wanachama wa taasisi ya Federation
waliojitolea kufanya usafi na kutoa elimu kwa ajli ya kutokomeza ugonjwa wa
kipindupindu katika manispaa ya Kinondoni iliyoko jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Covenant bank, Balozi
Salome Sijaona amesema kuwa benki hiyo imekuwa Msitali wa mbele katika
kuisaidia jamii ya Watanzania wasio katika sekta Rasmi ambao kwa kiasi kikubwa
ndio wanaoishi katika Mazingira magumu na hatarishi.
Hiki kipindipindu tunatakiwa kukiondoa kiwe tu kwenye vitabu vya historia kwamba enzi hizo kilikuwepo. Tujiwekee mikakati hatuhitaji kuwa nacho, kama ni elimu ya usafi tupewe kila mahali.
ReplyDelete