Waziri
Mkuu Mstafu Jaji Joseph Sinde Warioba akihutubia wakazi wa Butiama
ambapo aliwaeleza Magufuli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MARA
WAZIRI Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, ameibuka katika
kampeni za mgombea urais wa CCM Dk. John Magufuli na kusema kuwa
anashangazwa na hatua ya mawaziri wakuu wenzake kuhama CCM na kudai
hakuna kilichofanyika katika miaka 54 ya Uhuru.
Pamoja na hali hiyo amesema anajua wazi huenda hata
wanachokifanya hawajui wajibu wao walipokuwa katika madaraka hayo kama
washauri wakuu wa rais.alisema sasa umefika wakati wa watu
wanaomtumia kama dira Baba wa Taifa katika kampeni zao wajitafakari
zaidi.
"Wengine katika kampeni zao wanatumia maneno ya Mwalimu
kama wamechanganyikiwa. Huwezi kumtumia Mwalimu kama dira halafu unasema
CCM haijafanya kitu, aliijenga Tanzania kwenye misingi na wote
walimfuata wanapita kwenye misingi yake," alisema Jaji Warioba
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama
cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi
waliojitokeza katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika mjini Bunda
leo.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipokea kifimbo na Chief Japhet Wanzagi kwa niaba ya Wazee wa Butiama.
Dkt akionesha fimbo hiyo aliyokabidhiwa na Chief wa Wazanaki,Japhet Wanzagi
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama
cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge kulia ni
Nimrod Mkono kutoka jimbo la Butiama Vijijini na Profesa Sospeter
Muhongo ambaye anatoka jimbo la Musoma vijijini.
Mamia ya Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe
Magufuli. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...