Na Bashir Yakub
Hela ya mifuko ya hifadhi ya jamii ni hela ambayo mwajiriwa hukatwa kiasi kadhaa katika mshahara wake na mwajiri hutoa kiasi kadhaa na kuhifadhiwa katika mfuko uitwao mfuko wa hifadhi ya jamii. Mfuko wa hifadhi ya jamiii ni kama NSSF, PSPF, LAPF, GEPF n.k. Hii ndio mifuko ya hifadhi ya jamii. Ipo mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo huhudumia mashirika ya umma na ipo mingine ambayo huhudumia mashirika binafsi, makampuni binafsi na sasa ipo inayohudumia hata wajasiriamali wadogo ambao sio kampuni wala shirika.
Lengo kuu ni kumpunguzia mtumishi au mfanyakazi machungu ya maisha pindi anapostaafu au kuacha kazi. Ni kumwezesha mtu kuweza kukabiliana na maisha yake baada ya kutokuwa na kazi iliyokuwa ikimwingizia kipato. Ni kumfanya asikose hata matumizi ya kawaida kama chakula, malazi, mavazi na hata matumizi kama ada za shule ,matibabu n.k. Mifuko hii haipo Tanzania tu bali ni ajenda ya dunia. Ukienda ulaya, Amerika, Asia na kote Afrika utaikuta.
Naomba muwasiliane na SSRA kwani hizo taarifa CHANZO CHAKE SIO SSRA.
ReplyDeleteMifuko yote ya hifadhi ya jamii Tanzania hu hudumia Watanzania wote bila kujali ni mwajiriwa wa sekta ramsi au sekta isiyorasmi.