Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli(katikati) akiwanadi Mbunge wa Handeni Mjini Dk. Abdallah Kigoda (kulia) na Mgombea wa Ubunge Jimbo la Handeni Vijijini Ndugu Mboni Mhita kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Kigoda mjini Handeni.

Wakati kampeni za kuwania Urais,Ubunge na Udiwani zikidizi kushika kasi nchini,Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli,amesema atasimamia utawala wa sheria kwa kuwawajibisha wale wote wanaopindisha sheria kwa faida yao.

Magufuli aliyepewa jukumu la kuipeperusha bendera ya chama cha Mapinduzi,katika ngazi ya urais,amesema utawala wake hautakuwa na simile na wanaopoka haki za wanyonge,amesema kuwa ni jambo lisilokubalika kuona haki za wanyonge zikipokwa na matajiri wachache na kuelezea kuwa atawashughulikia kwa mujibu  sheria zilizopo.

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisoma bango la vijana wafanya biashara ndogo ndogo wa eneo la Dumila maarufu kama Feri wakati akielekea mkoani Tanga ikiwa muendelezo wa mikutano ya kampeni za CCM .

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa wasili katika kijiji cha Muheza-Masagala akielekea wilayani Handeni kuwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni
Baadhi wananchi wa kijiji cha Vyadigwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli (hayupo pichani) alipowahutubia wakazi wa kijiji hicho wilayani Kilindi
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili katika kijiji cha Muheza-Masagala akielekea wilayani Handeni kuwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni

Team Magufuli ya Handeni nayo ilikuwepo kuwahamasisha wananchi wampigie kura ya ushindi Dkt Magufuli,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kigoda.
Wakifuatilia mkutano wa kampeni ndani ya Mvomero .

Wananchi wa Handeni wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Kigoda mjini Handeni.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Turiani mkoani Morogoro na kuwaambia atahakikisha migogoro ya ardhi inamalizika na kuileta jamii kuishi kwa amani na upendo.

PICHA NA MICHUZI JR-HANDENI

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...